Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimwa Mhandisi Richard Ruyango, amewataka wananchi wilayani humo, kwenda kupata chanjo ya ugonjwa hatari duniani, unaosababishwa na virusi vya corona 19 (UVIKO 19), kutokana na ukweli kwamba chanjo hiyo ni salama na iimethibitishwa na watalamu wa afya kwa viwango vya kimataifa.
Mkuu huyo wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Ruyangwa ametoa rai hiyo wakati akizinduzi rasmi wa zoezi la chanjo ya ungonjwa wa virusi vya Corona 19 ( UVIKO 19) katika halmashauri ya Arusha, zoezi lililofanyika kwenye hospitali ya wilaya Olturumet na kuendelea kutolewa kwenye vituo vingine vitatu vilivyoainishwa katika halmashauri hiyo.
"Leo tumezindua chanjo ya UVIKO 19 katika wilaya yetu ya Arumeru, inayohusha wananchi wa halmashauri za Meru na Arusha, niwatake wananchi wangu, kutumia fursa hiyo iliyotolewa na serikali bila gharama yoyote licha ya kuwa serikali imetoa uhuru wa mtu kuamua kuchanja ama la, lakini ni vema kutambua kinga ni bora kuliko tiba" amefafanua Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo, wananchi wa halmashauri ya Arusha, wamejitokeza kwa wingi katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupata chanjo hiyo, bila kujali makundi matatu yaliyoanaishwa na serikali kuanza kuchanjwa, wakiwemo viongozi wa chama na serikali, viongozi wawakilishi wa wananchi, waheshimiwa Madiwani, viongozi wa dini na mila pamoja na watu wa rika mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha na Diwani wa kata ya Laroi, mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amewataka wananchi kutumia fursa hiyo adhimu iliyotolewa na serikali kwa kufanya maamuzi sahihi na kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa na kuchanja chanjo hiyo, kwa kuwa imethibitishwa na watalamu wa afya kupitia shirika la afya duniani na wizara ya afya, licha ya kwamba chanjo hiyo ni hiari.
"Ninaipongeza serikali kupitia Wizara ya Afya, kwa kutuletea chanjo ya ugonjwa hatari wa Corona, mimi kama kiongozi nimekuwa wa kwanza kuchanja katika halmashauri yangu, ili kuonyesha mfano kwa wananchi wangu, chanjo ni salama, hivyo wananchi wanatakiwa kuachana na maneno ya kwenye mitandao, watumie fursa iliyotolewa na serikali kuchanja, hata kama chanjo hiyo ni hiari "amesema Mheshimiwa Ojung'uNaye
Mzee wa ukoo, Laigwanani Boniface Tarakwa, amewataka wananchi kuacha kusikiliza maelezo ya uzushi yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba chanjo hiyo ina madhara mara baada ya kuchomwa, lakini maneno hayo hayana ukweli, kwa kuwa yeye amechanja na hajaona mabadiliko yoyote kimwili ni kama chanjo nyingine alizowahi kuchanja.
"Mimi nimechanja leo sijaona mabadiliko yoyote, maneno ya kwenye mitandao yanawajengea hofu, tafuteni taarifa shaihi kutoka kwa watalamu msikubali kupotoshwa kama ni chanjo tumesha chanja chanjo nyingi, tunapaswa kufuata maagizo ya watalamu wa afya ili kujikinga na gonjwa hili hatari la corona" amesisitiza Mzee wa Mila
Naye Steven Laiza (59) anayefanya kazi za Utalii, amesema kuwa rais amefanya jambo jema na la hekima sana, Tanzania sio kisiwa, tunamchangamano na nchi nyingine duniani, hatuwezi kwenda tofauti na nchi za wenzetu, ni muhimu serikali kuhakikisha inaleta chanjo za kutosheleza wananchi wote.
Hata hivyo Mganga Mkuu, halamshauri ya arusha, Dkt. Petro Mboya, amesema kuwa halmshauri ya Arusha imepata jumla ya chanjo 11,082, na kuainisha makundi maalumu yatakayopata chanjo hizo ni pamoja na wahudumu wa afya, walimu, watu wenye magonjwa sugu yasio ambukiza, watu wenye umri mkubwa wa kuanzia miaka 50 na kuwahimiza wananchi kujitokeza kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya, huku akibainisha vituo hivyo ni Hospitali ya Olturumet, Haospital ya Seliani Ngaramtoni, Kituo cha Afya Mduruma na Zahanati ya Ngorbob kata ya Matevesi eneo la Kisongo.
Aidha Dkt. Mboya amewasisitiza wananchi kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya kwa kunaa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barako, kuepuka misongamano isiyo ya lazima.Awali uzinduzi huo, umefanyika kufuatia agizo la Serikali kupitia wizara ya Afya, la wananchi kupata chanjo hiyo ya UVIKO 19 katika mikoa yote ya Tanzania.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa akichomwa sindano ya chanjo ya UVIKO 19, wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19, katika halmashauri ya Arusha, kwenye hospital ya wilaya ya Olturumeti
Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa akichomwa sindano ya chanjo ya UVIKO 19, wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19, katika halmashauri ya Arusha, kwenye hospital ya wilaya ya Olturumet
Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio akichomwa sindano ya chanjo ya UVIKO 19, wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19, katika halmashauri ya Arusha, kwenye hospital ya wilaya ya Olturumeti
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.