Na. Elinipa Lupembe.
Katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja, Benki ya NMB kanda ya Kaskazini, tawi la Clock Tower la Jijini Arusha, imedhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na halmashauri ya Arusha, kwa kuwezesha wakulima, wafugaji na wafanyabiashara ndogo wa halmashauri hiyo.
Dhamira hiyo imetolewa na Meneja wa Bank ya NMB Tawi la Clock Tower, Emmanuel Kishosha, wakati wa kikao cha pamoja kati ya wafanyakazi wa tawi hilo la NMB na timu ya Menejiment ya halmashauri ya Arusha, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Meneja wa tawi hilo la Clock Tower amesema kuwa, ni wazi kwamba Benki ya NMB ni benki ya serikali hivyo inawajibu wa kuwawezesha wananchi kiuchumi, hasa wakulima, wafugaji na wajasiriamali wadogo, ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali, kuelekea uchumi wa viwanda.
"Arusha DC ni wadau wetu wakubwa, tushirikiane kuawafikia wananchi mnaowahudumia, tuunganisheni nao kulingana na mahitaji yao, ili NMB iwawezesha kukuza mitaji yao kwa gharama nafuu, tofauti na benki nyingine za kibiashara, NMB benki inatoa huduma kwa wananchi wa hali zote, pale mnapokuwa na uhitaji, tuandikieni barua, tutashirikiana kwa huduma na misaada stahiki kadri tutakavyoweza, hilo ndilo jukumu la NMB bank". Amesisitiza Meneja Kishosha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, licha ya kuushukuru uongozi wa benki ya NMB tawi la Clock Tower kwa ushirikiano mkubwa wa kuwahudumia watumishi na wananchi wa halmashauri hiyo, ameomba benki hiyo kuendelea kuunga mkono, utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika halmashauri hiyo kwa kuchangia miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya na biashara.
"Mmekuwa mkitusupport sana, bado mmeona ni muhimu kuwa karibu zaidi na uongozi wa Arusha DC, jamii yetu inamahitaji mengi naamini tukishirikiana tutafikia lengo la serikali la kuwawezesha wananchi kukua kiuchumi na kutekeleza sera ya Viwanda na kukuza uchumi wa taifa letu"amesema Mkurugenzi Mtambule
Hata hivyo mkutano huo, uliambatana na zawadi mbalimbali zilizotolewa na NMB kwa timu hiyo ya menejimenti pamoja na keki kama ishara ya benki hiyo kusumisha ushirikiano na Halmadhauri ya Arusha.
Wiki ya huduma kwa Wateja imefikia kilele kwa taasisi zinazotoa huduma, kushiriki shughuli mbalimbali na wateja wanaowahudumia, huku taasisi hizo zikijipambanua shughuli na huduma zinazotoa kwa ubora zaidi ya nyingine.
l
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.