• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

OIKOS watoa msaada wa vifaa tiba vya mifugo Arusha DC

Posted on: February 21st, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Halmashauri ya wilaya  Arusha imepokea msaada wa vifaa tiba vya mifugo, kutoka shirika lisilo la kiserikali la OIKOS, shirika linalofanya shughuli zake ndani ya halmashauri hiyo, kwa kujihusisha zaidi na masuala ya Ardhi, Kilimo na Mifugo, kupitia mradi wa Eco - Boma, mradi unaofadhiliwa na nchibza Ulaya.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Dkt. Wilson Mahera, ameushukuru uongozi wa shirika hilo kwa  jitihada wanazofanya hasa katika kuwajengea uwezo wananchi wa halmashauri hiyo, shughuli ambazo ni msingi wa maendeleo kwa jamii ya wananchi wa halmashauri hiyo na taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa anatambua na kuthamini, mchango mkubwa unaotolewa na shirika la OIKOS, mchango ambao unaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, kutokana na kazi zinazofanywa na shirika hilo, kazi ambazo zinaonekana wazi,  kuwafikia wananchi wa hali ya chini na kuongeza, kuwa kazi hizo zina matokeo chanya kwa wananchi.

Aidha amewataka maafisa Ugani, kutumia vifaa hivyo kwa lengo lililokusudiwa, la kuwahudumia wafugaji na kuongeza kuwa ni vema maafisa Ugani hao kuwafuata wafugaji, katika maeneo yao na si kuwasubiri ofisini mpaka wafugaji wawatafute, huku akiwasisitiza kutoa huduma kwa weledi kwa kuzingatia sheria na  kanuni zinavyoelekeza.

"Ninataka vifaa hivi vitumike kutoa huduma stahiki kwa wafugaji na si vinginevyo, na zaidi wafuateni wafuga kwenye maeneo yao na si kuwasubiri wawafuate ofisini,toeni huduma kwa weledi huku mkizingatia kanununi na taratibu zinavyoelekezwa" amesema Kurugenzi Mahera.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja msaidizi mradi wa Eco Boma unaotekelezwa na shirika la OIKOS, Ifura Ukio amesema kuwa lengo la kutoa vifaa huvyo kwa halmashauri ni kuwawezesha maafisa ugani kutoa huduma ya chanjo kwa mifugo kwa urahisi, chanjo ambazo zitazuia magonjwa ya mifugo na kuimarisha afya ya mifugo.

Amesema kuwa shirika linatambua na kuthamini juhudi za serikali za kuimarisha zao la mifugo kuelekea uchumi wa viwanda, hivyo kuamua kuwawezesha watalamu kutoa huduma ya chanjo kwa ufanisi zaidi.

Ifura amevitaja vifaa vilivyokabidhiwa kwa halmashauri hiyo ni pamoja na Freezaer moja kwa ajili ya kuhifadhia chanjo, cool box 10, tano za ujaxo wa lita 10 na tano za ujazo wa lita tano kwa ajili ya kubebea chanjo kutoka kwenye stoo ya chanjo kwenda kwa wafugaji, pamoja na kutengeneza fiji kubwa ya halmashauri ambayo ilikuwa imeharibika.

Naye Daktari wa Mifugo halmashauri ya Arusha Dkt. Linus   amesema kuwa uwepo wa vifaa tiba hivyo utarahisisha kazi ya chanjo kwa Maafisa Ugani kwenye kata na vijiji, kutokana na ukweli kuwa ukosefu wa vifaa tiba.

Amefafanua kuwa, awali Maafisa Ugani walikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa tiba, jambo ambalo liliwalazimu baadhi ya Maafisa Ugani, kukodi au kununua cool box ndogo ili kuwezesha zoezi hilo la kutoa chanjo kwa mifugo huku wengine wakishindwa kumudu kununua vifaa hivyo.

Hata hivyo vifaa tiba hivyo vitagawiwa kwenye ofisi za kata, kwa ajili ya kurahisishia Maafisa Ugani wa vijiji  utoaji wa chanjo kwenye vijiji kwa  wafugaji wenye mifugo inayopatiwa chanjo za  magonjwa ambayo chanjo zake hutolewa kila baada ya miezi mitatu.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.