Na Elinipa Lupembe
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wamekutana na watumishi wa Makao Makuu, halmashauri ya Arusha, kwa lengo la kukumbushana majukumu na wajibu wa mfuko kwa watumishi pamoja na mabadiliko ya mfuko, ikiwemo kikokotoo cha mafao ya kustaafu.
Akizungumza kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, Afisa Mwandamizi PSSSF Kanda ya Kaskazini, Venance Mwaijibe, amesema kuwa, Mfuko wa PSSSF una jukumu la kuwahudumia watumishi wa Umma hivyo watumishi wanapaswa kuufahamu mfuko na huduma wanazostahili kupata wakiwa kwenye ajira na sio mpaka kustafu.
Mwaijibe ambainisha kuwa watumishi wengi hufika ofisi za PSSSF pindi wanapolazimika kuanza kufuatilia mafao ya kustaafu, jambo ambalo si sahihi, mtumishi anatakiwa kufika na kuufahamu mfuko mara anapoanza makato na kuendelea kufuatilia mpaka pale anapofikia muda wa kustaafu.
Aidha ameyataja mafao yanayotolewa na mfuko ni pamoja na uzee, uzazi, ugonjwa, ulemavu, kukosa ajira na warithi, na kufafanua kuwa baadhi ya mafao si lazima mtumishi awe amestaafu utumishi wa Umma.
Aidha ametoa ufafanuzi wa maana halisi ya kikokotoo cha asilimia 33 na kufafanua kuwa, kuanzia tarehe 01 Julai, 2022, mtumishi atakapostaafu atapatiwa fao la mkupuo la asilimia 33 na kuendela kupata fedha kwa mwezi kipindi chote cha maisha yake kwa kuzingatia kanuni za kikokotoo cha hesabu za mfuko.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji, amelishukuru shirika hilo kwa elimu waliyoitoa kwa watumishi, elimu ambayo imefungua wigo na uelewa mpana wa kufahamu wajibu wa mwajiri na haki za mtumishi, elimu ambayo inapaswa kutolewa mara kwa mara kwa watumishi ili kuondoa sintofahamu kwa watumishi walio wengi.
"Tumeleweshwa manufaa ya mfuko kwa watumishi pindi watakapostaa, na kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa watumishi wengi na kuuona mfuko kama ni unyonyaji jambo ambalo si sahihi, elimu hii ni muhimu na inapaswa kutolewa kwa watumishi mara kwa mara". Amesisitiza Msumi
Naye Mwanasheria wa Halmashauri ya Arusha, Mhudini Lesirwa, ameomba marekebisho ya sheria ya fao la uzazi kupatiwa wanaume pindi wenza wao, wanapojifungua kwa kuwa, wapo wanaume ambao ni watumishi lakini wenza wao si watumishi.
"Mfuko unapaswa kufikiria kutoa fao la uzazi kwa wanaume ambao wenza wao si watumishi, ili nao wafaidi mfuko huo sawa na wanawake, kwa kuzingatia kila mwanachama ana haki sawa bila kuzingatia jinsi yake". Ameweka wazi Lesirwa
Kikao kazi hicho, kimetoa nafasi kwa watumishi kuuliza maswali mengi na kupatiwa majibu, jambo ambalo limejenga uelewa wa pamoja kati ya wwatumishi na Mfuko hususani kwenye suala zima la kikokotoo.
ARUSHA DC
KaziInaendelea
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO KAZI
Afisa Mwandamizi PSSSF Kanda ya Kaskazini, Venance Mwaijibe, akizungumza na watumishi wa Makao Makuu halmashauri ya Arusha, kwenye kikao kazi cha kujadili masuala mbalimbali ya Mfuko wa PSSSF, kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, akizungumza na watumishi wa Makao Makuu halmashauri ya Arusha, kwenye kikao kazi cha kujadili masuala mbalimbali ya Mfuko wa PSSSF, kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Baadhi ya watumishi wa makao makuu halmashauri ya Arusha wakifuatilia mijadala juu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii PSSF wakati wa kikao kazi cha kujadili masuala mbalimbali ya Mfuko wa PSSSF, kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.