Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameipandisha hadhi Manispaa ya Mji wa Dodoma na kuwa Jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya.
Dkt. Magufuli amesema hayo, wakati akihutubia wananchi waliohudhuria kwa sherehe za maadhimisho ya sikukuu za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba, uliozaa Jamhuri ya Muungano Tanzania, zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri, Dodoma
“Lengo la Serikali kuhamia Dodoma lipo pale pale, na hatuwezi kurudi nyuma. Sasa hivi zaidi ya watumishi 3,800 wameshahamia, mimi nitahamia Dodoma mwaka huu" amesema mheshimiwa Rais.
Ameongeza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya nchi hivyo kwa mamlaka yake ameitangaza Manispaa ya Mji wa Dodoma kwa Jiji na kuongeza kuwa mkurugenzi wa wa Manispaa hiyo kuwa Mkurugenzi wa Jiji la
" Kwa mamlaka mliyonipa, natangaza rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2018, Manispaa ya Dodoma itakuwa Jiji la Dodoma, mkurugenzi wake ataanza kuitwa Mkurugenzi wa Jiji”, amesema Dkt. Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza mamlaka zinazohusika, kuanza maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hilo jipya na kulofanya Jiji hilo kuwa la kipekee kwa sababu lipo katikati ya Tanzania.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.