Na Angellah Msimbira
RAIS Samia Suluhu Hassan amemmwagia sifa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa kuwa ni bingwa wa mabadililiko.
Rais Samia ametoa kauli hiyo baada ya Mchengerwa na viongozi wengine wateule kuapa, katika hafla iliyofanyika leo Septemba 1, 2023 Ikulu Ndogo Zanzibar.
Amesema anachokihitaji kwa viongozi hao ni mabadiliko na kumtaja Mhe. Mchengerwa kuwa ni kiongozi bingwa wa mabadiriko.
“Tunachohitaji ni mabadiliko, kuna mabingwa wa mabadiliko na mmoja wao ni Mchengerwa, kwa mfano nilipomteua kwa mara ya kwanza kwenda utumishi alienda na kasi, kelele zikawa nyingi, nikasema labda waziri wangu kazidi kapandisha mabega nikampeleke michezo.”
“Kaenda michezo kazi aliyoifanya mmeiona, kaacha kazi nzuri sana katika michezo, nikampeleka utalii mipango aliyoiweka, Angella (Kairuki Waziri wa Malisili na Utalii) ukiifuata mipango iliyowekwa utalii unakwenda kupaa juu.”
Rais Samia ameongeza kuwa “sasa nimmepeleka TAMISEMI mwakani kuna kivumbi, na mimi nakujua najua unaweza, kivumbi kile kinafanana na kifua chako, najua unaweza kwa hiyo nimekupeleka tamisemi ni kazi kazi.”
Aidha, Rais Samia amesema kuwa mabadiliko aliyoyafanya si adhabu bali ni hatua ya kuimarisha utendaji kazi na kusisitiza kuwa anachohitaji ni uwajibikaji wa viongozi hao.
“Sisi ni watumishi na katika utumishi mahusiano ni jambo muhimu sana sasa, ukijipandisha na kutaka kukaribia mbinguni hutatumikia watu.”
“Nawaombeni sana upole si ujinga, upole wakati mwingine ni maarifa, unalifikiria jambo mara mbili mara tatu kabla hujatoa maamuzi kabla hujatoa karipio, nendeni mkawatumikie wananchi.”
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.