• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RAS ARUSHA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI KIUTU NA KUSISITIZA UKAMILISHAJI WA UJENZI..

Posted on: August 31st, 2022

Na Elinipa Lupembe

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Misseile Albano Musa, ametembelea na kukagua maendeleo ya  utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiutu, halmashauri ya Arusha, mradi unaotekelezwa na serikali kupitia program ya kuboresha elimu ya sekondari nchini (SEQUIP).

Katibu Tawala huyo, ameipongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango ambavyo ubora wa mradi unaonekana hata kwa macho licha ya kwamba mradi huo bado haujakamilika.

"Ninawapongea wa watalamu wa halmashauri ya Arusha, inaonesha namna gani mnafanyakazi kama timu, endeleeni kufanya hivyo ili kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi". Amesisitiza Katibu Tawala huyo.

Aidha amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halamashauri hiyo, kuhakikisha mradi huo  unakamilika kwa wakati ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wapangiwe shule hiyo na kuanza masomo ifikapo Januari 2023.

Awali akisoma Taarifa ya mradi huo, kwa niaba ya msimamizi wa mardi huo, na Makamu mkuu wa shule ya sekondari Kiutu, Mwl. Upendo Mollel, amesema kuwa mpaka sasa mradi umefikia asilimia 65 kukamilika na makadirio ya gharama za ukamilishaji wa mradi huo ni takribani shilingi milioni 250 fedha ambazo zikipatikana mradi utakamilika mpaka mwisho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amemshukuru Katibu Tawala huyo kwa kutembelea mradi huo na halmashauri yake kwa ujumla,  na kuahidi kutekeleza maagizo, yote aliyoyatoa lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapangiwa na kuanza masomo mapema mwezi Januari 2023.

Awali Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya arusha, Mwl. Menard Lupenza amesema kuwa, Serikali kupitia program ya SEQUIP ilitoa kiasi cha shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiutu, ujenzi unaojumuisha jengo la ghorofa mbili lenye kubeba vyumba 8 vya kadarasa, maktaba, maabara za masomo ya TEHAMA na  vyoo vya wanafunzi, jengo la Utawala na Maabara za masomo ya Kemia, Fizikia na Baiolojia.

"Mpaka kufikia mwezi Desemba, tunategemea kukamilisha vyumba vya 4 madarasa kwenye hii sakafu ya kwanza ya ghorofa, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze masomo mwaka ujao, majengo mengine yatakamilika kwa kuwa asilimia kubwa ya vifaa vifaa". Amesisitiza Afisa Elimu Lupenza

Hata hivyo baada y serikali kutoa kiasi hicho cha fedha, Diwani wa kata ya Kiutu mheshimiwa Malambo Malaki na wenziwe watatu walitoa eneo kwa ajili wa ujenzi wa shule hiyo kitoakana na ukweli kuwa watoto wa kata hiyo wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata masomo ya sekondari kwenye kata nyingine.


ARUSHA DC

TUPO KAZINI ✍✍

HAKIKISHA UMEHESABIWA


PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA UKAGUZI WA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONADRI KIUTU.


Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi (kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Misseile Albano Musa juu ya hatua ya utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kiutu.


Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Misseile Albano Musa wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kiutu.




Muonekano wa Maabara ya somo la Kemia katika shule ya Sekondari Kiutu.


Muonekano wa jengo la ghorofa mbili lenye vyumba nane vya madarasa, maktaba, maabara ya somo la TEHAMA na vyoo vya wanafunzi shule ya Sekondari Kiutu.`

Muonekano wa jengo la maabara ya masomo ya Kemia, Fizikia na Baiolojia shule ya Sekondari Kiutu.`


Muonekano wa jengo la Utawala  shule ya Sekondari Kiutu.`

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.