Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Misaille Musa, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi, miradi ambayo inaendelea kupunguza changamoto za upatikanaiji wa huduma kwa wananchi hususani waishio vijijini.
Katibu Tawala huyo, amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 katika sekta ya afya, elimu na maendeleo ya jamii, halmashauri ya Arusha.
Ametoa shukrani hizo huku akiwapongeza watumishi na wananchi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana katika usimamizi wa miradi hiyo yenye ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali kwa kutumia Force akaunti.
"Tunamshukuru sana mama Samia, kwa kutoa fedha nyingi za miradi, miradi ambayo kiuhalisia inakwenda kuwahudumia wananchi wa maeneo ya pembezoni wenye uhitaji, kukamilika kwa upanuzi wa kituo cha Afya Mwandeti kutasaidia kuhudumia wagonjwa pamoja na kuondoa vifo vya kina mama wajawazito na watoto".Amesisitiza Missaile.
Hata hivyo ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Arusha, kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kukamilisha maeneo madogo madogo yaliyosalia katika kukamilisha ujenzi jengo la mama na mtoto Mwandeti, ili na wananchi waanze kupata huduma kituoni hapo kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Katika ziara hiyo, jumla ya miradi minne ya ikiwemo miradi iliyotekelezwa na TASAF ya Kivuko cha Moivo shilingi milioni 67 .1 na ujenzi wa mabweni mawili shule ya sekondari Oldonyowas kwa shilingi milioni 356.
Aidha miradi mingine na paomja na ujenzi wa kituo cha afya Oloirieni milioni 450 za mapato ya ndani na upanuzi wa kituo cha Afya Mwandeti kwa shilingi milioni 590 kutoka serikali kuu ikiwa ni fedha za Uviko 19, tozo na wahisani.
ARUSHA DC
KaziIendelee✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.