Na Elinipa Lupembe.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Musa Massaile, amewashukuru wajumbe wa Kamati ya kusimamia ofisi ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakikishi Zanzibar, mara baada ya kukamilisha ziara yao ya kikazi mkoani Arusha.
Katibu Tawala huyo, amemewashukuru wajumbe hao kwa kuuamini mkoa wa Arusha na kubainisha kuwa ziara ya mafunzo ni muhimu kwa viongozi inayowapa fursa ya kubadilishana uzoefu wenye tija na kujionea nini wengine wanafanya katika kutekelza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya jamii na Taifa.
"Ziara hii ikawe chachu ya maendeleo na yenye tija kufikia malengo kwa maaendeleo ya wanachi katika maeneo yenu, tunajenga Taifa moja la watanzania hivyo umoja huu ndio utakaolifikisha Taifa hili mbele".Amesisitiza Katibu Tawala huyo
Aidha amefafanua kuwa miradi waliyotembelea ni sehemu ndogo sana ya miradi iliyotekelezwa katika mkoa wa Arusha na kuongeza kuwa, serikali ya awa,u ya sita imetoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo katika halmashauri zote saba za mkao wa Arusha.
Hata hivyo wajumbe hao, wameushukuru uongozi wa mkoa wa Arusha hususani wilaya ya Aruemru kwa mapokezi mazuri lakini pia kwa utekelzaji imara wa miradi ya maendeleo, miradi ambayo wameshuhudia wenyewe namna wananchi wakieleza kunufaika kwayo.
"Tunawapongeza mkoa wa Arusha, tumeona namna wanachi wake wakiwa bizy kufanya kazi, tumeshuhudia ukarimu wao kwa wageni lakini zaidi tumeshuhudia namna serikali imewagusa wananchi wa hali ya chini moja kwa moja huku wananchi wakithibitisha hilo kwa hisia kali" Amefafanua Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Machano Othman Said
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.