Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaile Musa, amewataka watumishi kufanya kazi kwa weledi kwa kushirikiana pamoja kama timu, ili kufikia lengo la halmashauri na serikali kwa ujumla la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Katibu Tawala huyo, ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri ya Arusha na kupata fursa ya kuzungumza na watumishi wa Makao Makuu, ikiwa na lengo la kukumbushana namna bora ya utekelezaji wa majukumu kwa watumishi wa Umma.
Katibu Tawala Missaile ameweka wazi kuwa licha ya kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na watumishi wa halmashauri hiyo na kuufanya mkoa wa Arusha kuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri nchini, amewasisitiza kuendelea kuwajibika ipasavyo bila kukata tamaa.
Aidha amebainisha kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza kukwamisha utekelezaji wa majukumu, amewahimiza kutumia rasilimali zilizopo na kuendelea kishirikiana kama timu moja, kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Arusha wanapata huduma kupitia wao kama ilivyo lengo la serikali.
"Nafahamu kuna changamoto nyingi lakini zisitukwamishe wala kutukatisha tamaa, tuzigeuze kuwa fursa, niwasisitize kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi wa Umma, tumieni taaluma zenu kwa kushirikiana kwa sekta zote kwa kuwa kila sekta zote inategemea sekta nyingine" Amesisitiza Maiselle
Hata hivyo watumishi halmashauri ya Arusha, wamepata fursa ya kuelezea changamoto zinazowakabili, katika kutimiza majukumu yao, na kumuamba katibu Tawala kushughulikia zile zilizo ndani ya uwezo wake jambo ambalo litaongeza ari ya wawatumishinkufanya kazi.
Naye Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amemshukuru katibu Tawala huyo na kuahidi kutekeleza maagizo yote ikiwa ni pamoja na kuwasimamia watumishi kutekelza majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia taratibu za utumishi wa Umma.
"Watumishi hawa wanapambana sana kuhakikisha huduma kwa wananchi zinapatikana na zaidi tunamshukuru Rais wetu mama Samia Suluhu kwa kuboresha maslahi ya watumishi, ikiwemo kupandishwa kwa madaraja kwa watumishi wote ambao walikuwa wanastahili, nikuahidi hatutamuangusha mheshimiwa Rais". Amebainisha Mhandisi Ruyango
Awali katika ziara hiyo, licha ya kuzungumza na watumishi, katibu Tawala ametembelea miradi mimnee ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu na miundombinu ya barabara.
ARUSHA DC
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.