Na. Elinipa Lupembe.
Jumla ya mikataba 18 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.07 imesainiwa na wakandarasi wa kutengenza barabara za mkoa wa Arusha, huku Mkuu wa Mkoa wa huo Mhe. John Mongella akiwataka wakandarasi waliosaini mikataba hiyo, kufanya kazi kwa weledi, uzalendo na kuzikamilisha kwa muda uliopangwa kulingana na mikataba hiyo.
Mhe. Mongeka ameyasema hayo wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba kati ya Wakala wa barabara vijijini na Mijini ( TARURA) na wakandarasi 18 watakaofanya matengenezo barabara kwenye halmashauri za Mkoa wa Arusha.
"Tumesaini mikataba, wakandarasi tambueni fedha hizi ni za Umma, ni kodi za wananchi, Seriklai imewaamini na kuwapa kazi, nendeni mkatengeneze barabara zenye viwango, vinavyoendana na tahamani ya fedha na kukamilisha ujenzi kwa wakati kulingana na mikataba mliyoisaini" . Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Aidha Mongela amebainisha kuwa kukamilisha barabara hizo kwa wakati na kwa viwango kutasaidia kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kushusha gharama za maisha kwa wananchi na kuharakisha maendeleo binafsi na ya Taifa kwa ujumla na kuwaelekeza TARURA kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi hao kwa ukaribu zaidi ili kazi zifanyike kwa welesi na kukamilisha miradi hiyo kulingana na mikatana yao sambamba na kuendelea kusimamia miradi ya barabara ya zamani ili nayo iweze kukamilika haraka.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amesema, kuwa kitendo cha wakandarasi kusaini mikataba hadharani kitasaidia wananchi kuwafahamu wakandarasi watakaoenda kufanya kazi katika maeneo yao.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha Lynas Sanya amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamepatiwa jumla ya shilingi bilioni 4.07 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa awamu ya pili huku awamu ya kwanza ikipokelewa shilingi bilioni 14 na jumla ya shilingi bilioni 18.07 na jumla ya mikataba 34 ilisainiwa.
Nae, Mkandarasi Rashidi Sevingi kutoka kampuni ya Raly (EA) Limited ameahidi kwenda kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia mikataba waliyosaini na kuwasihi wakandarasi wote kufanya hivyo ili serikali iendelee kuaminiwa zaidi na kuendelea kuwapa kazi.
Awali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 TARURA katika bajeti yake wamepatiwa zaidi ya bilioni 10 fedha zilizotokana na tozo za mafuta ili zikasaidie katika ukarabati wa barabara katika Mkoa wa Arusha na kusaini Mikataba 52 yenye thamani ya bilioni 18 kwa ajili ya ukarabati wa barabara mbalimbali za Mkoa wa Arusha kwa mwaka wa fedha 2022/2023..
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.