Na Elinipa Lupembe
"Ninawaagiza viongozi wote wa Wilaya, Halmashauri, Wakuu wa Idara wa Mkoa wa Arusha, kwenda kukagua maeneo yote ili kujiridhisha na mwenendo mzima wa zoezi ka Sensa yaWatu na Makazi kabla ya tarehe ya mwisho."
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipokuwa akikagua zoezi la Sensa ya watu na Makazi katika Wilaya ya Longido na kujionea mwendendo mzima wa zoezi la Sensa katika mkoa huo.
Hata hivyo RC Mongella amebaini kuwa kuna baadhi ya maeneo makadirio ya kaya yalikuwa chini na mengine zaidi, hivyo amewataka viongozi wa Wilaya na Halmashauri zote kuyabaini maeneo hayo na kuchukua hatua haraka za kuhakikisha kaya hizo zinahesabiwa.
Amefafanua kuwa lengo la Mkoa wa Arusha, sio tu kumaliza zoezi la Sensa kwa muda uliopangwa bali kuhakikisha kaya zote ndani ya mkoa zimehesabiwa.
Aidha, amewaagiza viongozi wa makarani kuhakikisha, kwa makarani wanaomaliza kuhesabu katika maeneo yao mapema, wapangiwe maeneo mengine ambayo yanauhitaji zaidi ili kaya zote ziweze kufikiwa na kukamilisha kazi hiyo.
Naye Frida Mchome Karani wa Sensa Wilayani Longido, amesema kuwa kwa upande wake, zoezi la Sensa limeenda vizuri na amefanikiwa kuhesabu kaya 70 na baada ya kukamilika na kuhamishiwa kwenye eneo jingine.
Frida amebainisha changamoto kubwa aliyokutana nayo ni kutowakuta nyumbani baadhi ya wanakaya, kwasababu ya majukumu yao ya kikazi hivyo kupelekea kufanya zoezi la Sensa kulifanya hadi usiku.
Samweli Steven ni miongoni mwa wananchi waliohesabiwa na amesema zoezi la Sensa ni nzuri kwani litasaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo na amemshukuru Rais Samia kwa kuleta zoezi hilo.
RC Mongella anaendelea na zoezi la kufuatilia mwenendo mzima wa sensa ya watu na makazi katika halmashauri za Mkoa na kutatua changamoto zinazokuwa zimejitokeza katika maeneo hayo.
HAKIKISHA UMEHESABIWA✍✍
SOURCE: RC MKOA ARUSHA Facebook
Karani wa Sensa Halmasahuri ya Longido Frida Mchome, akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa ya kufuatilia maendeleo ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mkoa wa Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, akiwa kwenye moja ya kaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido, wakati wa ziara ya kikazi ya kufuatilia maendeleo ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mkoa wa Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, akiwa kwenye ziara ya kikazi Wilayani Longido kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mkoa wa Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.