Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Idd Kimanta, amewataka viongozi wa vijiji na vitongoji wilaya ya Arumeru, wanaoishi kwenye maeneo ambayo miundombinu ya Reli ya Arusha - Moshi inapita katika maeneo hayo, kusimamia na kuhakikisha usalama wa reli na miundombinu yake pamoja na usalama wa treni, mizigo na abiria wake.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai hiyo, alipokutana na viongozi wa ngazi zote, wanaoishi kwenye maeneo ambayo reli ya Moshi - Arusha, kwenye kikao kilihofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru, na kuweka wazi kuwa, matumizi ya Reli hiyo na safari za treni zinatarajia kuanza safari zake mwishoni na mwezi huu wa Agosti.
Aidha amewasisitiza viongozi hao kuzungumza na wananchi wao, ujio wa treni unotrji kufanya safari zake kutoka Dar es salam, Tanga, Kilimanjaro mpaka Arusha, safari ambazo zilisimama kwa zaidi ya miaka 20 sasa, na zinategemea kuanza kazi rasmi mwisho wa mwezi wa Agosti 2020 kw kuwa matengenezo yako kwenye hatua za mwisho kukmilika.
"Serikali ya awamu ya tano, imeona umuhimu wa kufufua safari za treni hususani Reli yetu ya Arusha - Moshi, ili kusaidia wananchi wa maeneo yetu, kusafiri na kusafirisha kwa gharama nafuu, na ni jukumu letu kuitunza, kuipenda na kutambua kuwa reli hiyo ni mali yetu sote, inatengenezwa kwa kodi zetu watanzania, kuitunza ni haki na wajibu wetu" amesema Mheshimiwa Kimanta
Safari za treni zitapunguza gharama kubwa za usafiri wanazotumia wasafiri wa kawaida na wafanya biashara, kutokana na ukweli kuwa treni inauwezo wa kubeba tani 800 za mizigo kwa wakati mmoja sawa na malori 80 kwa siku.
Ameongeza kuwa ujio wa reli utapunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara za lami, barabara zinazotumia pesa nyingi na kuharibika kwa muda mfupi matumizi yasiyosahihi ya magari kubeba mizigo mizito, matumizi ya reli ni maendeleo kwa uchumi wa Tanzania.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Shirika la Reli Tanzania 'TRCA', Jamila Mbaruku, ameweka wazi kuwa, ukarabati wa miundombinu ya reli ya Arusha - Moshi, unaendelea vema, uko katika hatua za mwisho, na safari za treni za mizigo na abiria zinatarajiwa kuanza kazi mapema mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti.
Aidha amewasisitiza viongozi hao, kuwatahadharisha wananchi wao, kuchukua tahadhari kwa kuacha kufanya shughuli za kijamii kwenye meneo ya karibu na reli, na kuongeza kuwa wazazi wanalazimika kuwatahadharisha watoto kucheza kwenye maeneo yaliyokaribu na reli.
"Tunafahamu reli hiyo ilikuwa haitumiki kwa muda mrefu sasa, watu wengi wamejisahau na kufanya shughuli zao karibu na reli, watu hao wanatakiwa kuacha mara kufanya hivyo na kufahamu ni hatari kubwa inayoweza kuhatarisha maisha" amesisitiza Jamila.
Hata hivyo viongozi hao, wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha wa kuwashirikisha ujio wa safari hizo za treni licha ya kwamba, italeta maendeleo ya Taifa lakini ni ukweli usiopingika wananchi wengi hawana uwelewa wa reli hizo, na wako tayari kuelimisha wananchi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.