Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amezungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mringa kata ya Oloirieni halmashauri ya Arusha, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa mabweni shuleni hapo.
Mhe.Mongella amewataka wanafunzi hao, kutumia fursa adhimu waliyo nayo kwa kusoma kwa bidii na kufafanua kuwa, serikali inawekeza fedha nyingi kwenye sekta ya elimu ili wanafunzi wasome vizuri, kwa kuwa serikali inahitaji watalamu wa fani mbalimbali kutoka kwao.
Amesisitiza wanafunzi hao licha ya kuzingatia masomo yao, wanatakiwa kujitambua na kujiepusha na makundi yenye kuendekeza tabia mbaya kwa kuwa na nidhamu ya maisha, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kumcha Mungu, kwa kuzingatia hayo wanaweza kufikia malengo na ndoto zao.
"Kazi ya mwanafunzi ni kusoma, hivyo soma kwa bidii, tumia muda wako vizuri ili uje kulitumikia Taifa lako, tambueni kuwa Taifa linawategemea, hata sisi tulikuwa wanafunzi kama ninyi na sasa tunafanya kazi za serikali, hakikisheni mnazifikia ndoto zenu, hakuna muujiza zaidi ya kujitoa na kujituma, wacheni tabia za hovyo kwa kuwa sio ujanja bali ni ujinga" .Ameweka wazi Mhe. Mongella.
Awali Mhe. Mongella ha
kusita kuwapongeza walimu na watumishi wasio walimu wa shule hiyo ya sekondari Mringa, licha ya changamoto za nyingi zinazoikabili sekta ya elimu lakini bado shule inafanya vizuri kitaaluma kwa kutoa wanafunzi wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kimkoa na kitaifa
Hata hivyo wanafunzi wa shule hiyo wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwatembelea na kuahidi kufanyia kazi yote aliyowaelekeza kwa kuwa wanaamini ndio msingi wa mafanikio yao ya baadaye.
Dorine Mwangamila, mwanafunzi wa kidato cha tano, ameishukuru serikalli kwa kuwajengea na kukarabati mabweni, kwani yalikuwa machache na mengine yalikuwa mabovu, na kusababisha wanafunzi kurundikana kwenye mabweni hayo machache na kuahidi kusoma kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri masomo yao.
Naye Peter Innocent kidato cha II, amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa namna alivyowahusia wanafunzi na kuthibitisha kuwa ni wamepata bahati ya kipekee, mkuu wa mkoa kuzungumza nao kama mzazi, maneno licha ya kuyafanyia kazi zaidi yataishi mioyoni mwao.
"Tunamshukuru mkuu wa mkoa kwa kupata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi, inaonesha namna gani anatujali, tunamuahidi hatutamuangusha, tutazingatia nidhamu ya maisha, kusoma kwa bidii pamoja na kumheshimu na kumcha Mungu". Amesema Peter
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
#KaaiInaendelea
PICHA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.