• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Shirika la RENEAL laimarisha somo la TEHAMA shule za sekondari Arusha DC

Posted on: August 30th, 2018

Somo la teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA limezidi kuimarika katika shule za sekondari 14 za halmashauri ya Arusha baada ya wafadhili kusimamia na kutoa kompyuta kwa shule hizo.

Uimara huo umetokana na ufadhili thabiti wa shirika lisilo la kiserikali la  Reneal Intanatinal Education Outreach la nchini Marekani kufadhili ufundishwaji na uendeshwaji wa somo la TEHAMA katika shule hizo.

Kwa kipindi cha takribani miaka mitano  sasa kuanzia mwaka 2013, Shirika hilo limewezesha uwepo wa Maabara za Kompyuta kwenye shule 14 na kutoa kompyuta 300 na viambata vyake kwa awamu tofauti huku idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hizo wakifaidika.

Akizungumza wakati wa kufungua maabara mpya ya komputa kwenye shule ya sekondari Sokon II na kukabidhi komputa 17 za maabara ya shule hiyo, mkurugenzi na mwanzilishi wa shirika hilo,  Bibi Rene Bierbaum amesema kuwa, wanafarijika sana kuendelea kutoa vifaa hivyo kwenye shule za sekondari katika halmashauri ya Arusha, kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa uongozi wa halmashauri hiyo, usimamizi imara wa komputa hizo shuleni pamoja na mwamko wa wanafunzi kutumia komputa hizo kama zana za kujifunzia.

Bibi Rene ameongeza kuwa, katika awamu hii ya mwisho, Reneal imetoa jumla ya Komputa mpakato 68, Kwa mgao wa kompyuta 17 kwa kila shule kwa shule nne za sekondari za Skon II, Kiranyi, Kimnyaki na Oldonyosambu, na kuongeza kuwa komputa 47,  zimeongezwa kwenye shule ambazo zilipata mwanzo na baadhi kubadilishwa zile ziliokaa kwa muda mrefu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera, licha  ya kulishukuru na kulipongeza shirika la RENEAL kwa msaada huo, amewataka walimu na wanafunzi kuzitunza  kompyuta hizo na kusisitiza kutumika hasa kwa ajili ya kujifunzia mambo muhimu ya kimasomo pamoja na kuhakikisha zana hizo zinaleta matokeo mazuri kwenye mitihani yao ya ndani na ile ya taifa.

Hata hivyo amefafanya kuwa mkakati wa halmashauri ni kuhakikisha shule zote za sekondari zinakuwa na maabara za Kompyuta ili kuwezesha wanafunzi wote kufanya mitihani ya Taifa ya somo la TEHAMA kuwa na ufaulu wa juu wa somo hilo na kuwa wabobezi katika matumizi ya kompyuta.

"Ingawa tunakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule zetu, mkakati wetu ni kushirikiana na wadau Reneal na wadau wengine kuhakikisha ifikapo mwa 2020 shule zote 27 za sekondari kuwa na maabara za kompyuta na wanafunzi wote kuweza kufanya mitihani ya Taifa ya kidato cha pili na cha nne kwa somo la TEHAMA huku wakiwa na uwezo mkubwa wa kutumia kompyuta" amesema Mkurugenzi Mahera.

Mkuu wa shule ya Sekondari Sokon II,mwalimu Mwamvita Kilonzo, amethibitisha kuhakikisha kompyuta hizo, zinatumika katika matumizi sahihi kwa wanafunzi kwa kujikita zaidi katika kujifunza kutumia kompyuta, kujifunza somo la TEHAMA na kutumia kama zana ya kujinzia kwa kupata Nukuu za mosomo mengine kupitia mtandao wa intaneti huku akisisitiza kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wanaunzi watakaotumia kompyuta hizo.

Naye Mratibu wa mradi huo wa maabara za Kompyuta shule za sekondari na Afisa TEHAMA, halmashauri ya Arusha David Nyangaka, amesema kuwa Kompyuta hizo, hazitakuwa na mfumo wa mitandao ya kijamii bali zimejazwa mambo ya muhimu yanayohusiana na masomo ya sekondari hivyo kuwafanya wanafunzi kutumia kwa ajili ya masomo zaidi na maarifa mengine ya ziada yanayoendana na maadili ya kitanzania na si vinginevyo.

Mkurugenzi Mtendaji Dk. Wilson Mahera kushoto, mkuu wa shule sekondari Sokon II mwalimu Mwamvita Kilonzo pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Sokon II mheshimiwa Melau Mollel wakizitazama baadhi ya kompyuta mpakato mara baada ya kukabidiwa na wadau wa shirika la Reneal.

Mkurugenzi na mwanzilishi wa shirika la RENEAL INTERNATIONAL EDUCATION OUTRICH BibiRene Bierbaum akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Sokon II.

Wakurugenzi na waanzilishi wa shirika la RENEAL INTERNATIONAL EDUCATION OUTRICH Bwana Neal Bierbaum na Bibi Rene Bierbaum wakimkabidhi kompyuta mpakato Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera.

 

Wanafunzi wa shule ya sekondari Sokon II wakicheza ngoma ya kabila la Kimaasai, wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa maabara mpya ya kompyuta pamoja a kukabidhiwa kompyuta na shirika la Reneal.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Sokon II wakiwa kwenye maabara yao mpya ya kompyuta mara baada ya kufunguliwa na kukabidhiwa kompyuta 17 na shirika la Reneal International Education Outrich.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.