Na Elinipa Lupembe
Fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF na mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, zimeanza kuzaa matunda kwa kuwawezesha wanufaika wa mpango huo, kuanzisha biashara ndogo ndogo na kujikimu na hali ngumu ya maisha.
Wanufaika hao, wamekutwa na mwandishi wetu, wakiwa kwenye biashara ya nguo za mitumba, wakati wa kupokea ruzuku ya fedha za ruzuku kwa mwezi wa 7/8 mwaka 2022, kwenye ofisi ya Kijiji cha Laroi kata ya Laroi, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Aidha wanufaika hao wameelezea hisia zao kwa serikali kupitia TASAF, namna imezitoa kaya hizo kwenye hali ngumu ya kiuchumi ya kushindwa kumudu hata kupata mahitaji ya lazima kwa familia zao, na kuongeza kuwa kwa sasa wameanza kusahau mateso hayo.
"Tunamshukuru Mungu, tunamshukuru Mama Samia, ameleta neema kwa kina mama, amekuwa ni mfano kwa kina mama, kila mama anajiamini kupitia Mama Samia, kama Rais anafanya kazi kwa nini sisi tusifanye, hakuna mwanamke analala siku hizi, TASAF imetutoa gizani". Wameweka wazi kina mama hao
Zaina Ebeneza (32) mnufaika wa TASAF kijiji cha Laroi na mama wa watoto watano, amebainisha kuwa amekuwa akopokea ruzuku ya shilingi 54,000, fedha iliyomuinua kutoka kwenye lindi la umaskini uliokithiti na kumuwezesha kupata mtaji wa kuuza nguo za mitumba.
"Ninauza nguo kwa kutembeza lakini pia ninauza kwenye minada siku ya soko, TASAF imenitoa mbali sana, nilikuwa na hali ngumu sana kimaisha, nina watoto watano wananitegemea, kwa sasa hali yangu imeimarika, ninafanya biashara yangu na ninapata mahitaji ya familia, watoto wanasoma na kupata mahitaji yao kama watoto wengine". Amesema Zaina
Naye Ester Lobulu ( 50) mfanyabiashara wa nguo na mbogamboga, amesema kuwa analea watoto na wajukuu watatu, mmoja ni yatima, ruzuku ya TASAF imemsaidia kufanya biashara nguo, siku za soko la Mirongo, nasiku za kawaida huuza mboga kwa kutembeza majumbani.
"Tunamshukuru Mungu, tunamshukuru mama Samia, TASAF imetusaidia hasa wamama, tulikuwa tunateseka na maelezi ya familia, mume aliniacha na akaniachia watoto, ninawasomesha, maisha sio magumu sana kwa sasa ninapambana na Mungu ananisaidia, siku za mnada nauza nguo Mirongoine, siku za kawaida natembeza mboga kwenye nyumba za watu". Amesema Ester.
Ifahamike kuwa Mpango wa kunusuru kaya masikini unalenga kuziwezesha kaya kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kupambana na adui ujinga, umasikini na maradhi kupitia ruzuku ya msingi ya kuiwezesha kaya kupata mahitaji ya chakula na mavazi, ruzuku ya elimu ya kuhakikisha watoto wa kaya wa kuanzia miaka 7- 18 wanapata elimu ya msingi huku watoto wa miaka 0-5 wanapata huduma za afya kwa kuhudhuria kliniki nankupata chanjo kwa kipindi chote.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
PICHA ZA WALENGWA WAKIWA KWENYE BIASHARA ZAO
Ester Lobulu (50) mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya masiikini, wa kijiji cha Laroi kata ya Laroi akiwa kwenye biashara yake ya kuuza nguo mtaji ambao amekiri kuupata kutokana nanfedha za ruzuku anayopikea kutoka TASAF.
Ester Lobulu (50) mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya masiikini, wa kijiji cha Laroi kata ya Laroi akiwa kwenye biashara yake ya kuuza nguo mtaji ambao amekiri kuupata kutokana nanfedha za ruzuku anayopikea kutoka TASAF.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.