Na Elinipa Lupembe.
Licha ya kuwa Serikali inaendelea na mkakati wa kukarabati shule kongwe za sekondari bado imejikita katika kuziimarisha shule changa kwa kuongeza miundo mbinu ili zikamilike, lengo likiwa ni kuhakikisha watoto wote nchini, wanapata elimu ya sekondari katika maene yao.
Shule ya sekondar Losinoni ni miongoni mwa shule changa za kata iliyoanza mwaka 2020 kwa kuusajiliwa kwa namba S. 5347, ikiwa umbali wa takribani Kilomita 45 kutoka makao makuu ya halmashauri ya Arusha.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mkuu wa shule ya sekondari Losinoni Mwl. Emanuel Mkonongo, amethibitidha kuwa serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo huku mwaka huu wa fedha ikiwa imepokea shilingi Milioni 40 kutoka serikali kuu za ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, viti na meza 80 na kufanikiwa kujenga na ofisi ya walimu kwenye jengo hilo na ujenzi ukiwa umekamiliaka.
Imeelezwa kuwa, shule hiyo ilianzishwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa Hifadhi ya Wanyamapori Arusha (ANAPA) kutokana na asilimia kubwa ya watoto wa eneo hilo hususani wasichana kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na umbali mrefu ilipokuwa shule ya sekondari.
Kutokana na juhudi na ari ya wananchi wa Losinoni, serikali ilianza kuwekeza nguvu na kuongeza kasi ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule hiyo pamoja na usajili wa shule hatimaye Januari 2020, wanafunzi walipangiwa shuleni hapo kuanza kidato cha kwanza.
Mkonongo ameongeza kuwa, Serikali imeendelea kuwekeza miundombinu ya shule hiyo na kuifanya iendelee kukua kwa manufaa ya watoto wa kijiji cha Losinoni, mpaka sasa shule ina wanafunzi 202 wa kidato cha kwanza mpaka cha tatu ikiwa na vyumba 10 vya madarasa, matundu ya vyoo, maabara za masomo ya Kemia na Baiolojia, na Fizikia na Jiografia, pamoja na nyumba 2 za walimu za (2 in 1).
"Licha ya kuwa shule hiyo ni changa lakini juhudi kubwa za serikali zinaifanya shule hiyo kuwa bora kwa upande wa miundo mbinu, huku wadau wengine wa maendeleo wakiendelea kutoa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ikiwemo wanafunzi wasomi wenyeji wa kijijini hapo" Amesisistiza Mkonongo
Awali Serikali imetoa shilingi milioni 760 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 38 kwa 15 za sekondari halmashauri ya Arusha, ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2023.
Ifahamike kuwa, mradi huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 79 kifungi (i) ikijibainisha kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya sekondari kwa kuongeza idadi ya shule za sekondari, kuboeresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi lengo likiwa kuongeza ufaulu wa wananfunzi wa kidato cha nne.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.