Na. Elinipa Lupembe.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetoa pikipiki 48 kwa Maafisa Kilimo, halmashauri ya Arusha, ikiwa ni vitendea kazi kwa Maafisa hao, lengo likiwa ni kuboresha sekta ya Kilimo nchini.
Akizungumza wakati akikabidhi pikipiki hizo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amewaagiza Maafisa Kilimo kuhakikisha wanatumia pikipiki hizo, kutekeleza majukumu yao kama yalivyo makusudio ya serikali na si vinginevyo.
" Serikali inathamini kazi kubwa mnayoifanya na kuwapa vyombo hivi vya usafiri ili kuwarahisihia utekelazaji wa majukumu yenu kwa wakulima, hatutegemei kuwakuta ofisini, ni jukumu lenu sasa kuwafuata na kuwafikia wakulima kwa haraka na kwa wakati, tunategemea matokeo chanya kwenye sekta ya kilimo katika wailya yetu." Amesisitiza Mhandisi Ruyango.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojun'gu Salekwa, amekiri kufarijiwa na serikali ya awmu ya sita, kuwapatia maafisa Kilimo vyombo hivyo vya usafiri, kutokana na mazingira magumu wanayofanyia kazi na kusisitiza kutegemea matokeo chanya kwenye sekta ya kilimo kati halmashauri hiyo.
Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji halmasahuri ya Arusha, Seleman Msumi, amewahimiza maafisa hao, kutambua kuwa wamepewa vyombo hivyo vya usafiri kama dhamana, ni muhimu kuvitunza na kuvitumia kwa kazi ya kuwahudumia wakulima katika maeneo yao.
Awali Maafisa ugani hao, wamemshukuru mheshimiwa rais mama Samia Suluhu na kuipongeza serikali yake ya awamu ya sita kwa kuwapatia pikipiki, ikiwa ni kitendea kazi muhimu kwao, kitakachowarahisishia utekelezaji wa majukumu yao hususani kuwafikia wakulima kwa urahisi zaidi.
Afisa Kilimo kata ya Bwawani, Charles Lyakurwa licha ya kumshukuru mama Samia, amebainisha kuwa pikipiki hiyo ni kitendea kazi muhimu sana kwake, kwa kuzingatia kata yake ya Bwawani ina wakulima wengi wenye mashamba makubwa ambao wanahitaji huduma kutoka kwake kama mtaalamu, bila usafiri wa uhakika ilikiwa ni changamoto kuwafikia kwa wingi wao.
Judith Malya Afisa Kilimo kata ya Ilkiding'a amesema kuwa, awali iliwalazimu kutembea hadi umbali wa Kilomita 20 kuwafuata wakulima, uwepo wa pikipiki utarahisisha na kuwafikia wakulima kwa wakati.
Awali Kiamu Mkuu wa Idara ya Kilimo, halmashauri ya Arusha, Bahati Mtweve, amefafanua kuwa jumla ya pikipiki 48 zimekabidhiwa na serikali kupitia wizara ya Kilimo na kukabidhiwa maafisa Ugani wote 48 kwa majina yao ndani ya halmasahuri, lengo likiwa kuboresha sekta ya kilimo nchini.
KaziInaendelea✍✍
JIANDAE KUHESABIWA
Afisa Kilimo kijiji cha Oloigueruno, Grace Mdaha ( wa kwanza kushoto) akipokea ufunguo wa pikipiki tayari kwa kwenda kuanza kazi, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango ( wa kwanza Kulia) , zoezi lililofanyika kwenye ofisi za Makao makuu ya Halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.