Na. Elinipa Lupembe.
Kufuatia mkakati wa serikali wa kuboresha miundombinu ya vituo vya kutolea huduma ya afya, wananchi wa kata ya Oldonyosambu, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, wameendelea kuneemeka kwa kupatiwa mradi wa upanuzi wa kituo afya Oldonyosambu.
Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 200, fedha kutoka serikali kuu, kupitia miradi ya Lipa kwa na Matokeo 'Result based financing', unategemea kukamilika mwishoni mwa mwaka huu 2021.
Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewataka watalamu wasimamizi wa mradi huo, kuhakikisha unakamilika kwa wakati huku ubora wa majengo ukienda sambamba na thamani ya fedha za mradi.
Mkurugenzi Msumi ameongeza kuwa, mradi huo ni muhimu kwa wananchi wa Oldonyosambu, kwa kuzingatia malengo ya serikali ya awamu ya sita, ya kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma hizo muhimu, karibu na wanachi, kwa kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye hadhi ya nyota tano, huku kila kijiji kikiwa na Zahanati.
Afisa Mipango halmashauri hiyo, Anna Urio, amefafanua kuwa kiasi hicho cha shilingi milioni 200, kinategemea kutumika kujenga jengo moja kubwa, litakalojumuisha, wodi ya mama na mtoto 'maternity ward', sehemu ya kujifungulia 'labour word', sehemu ya upasuaji 'theater' na RCH, lengo likiwa ni kuongeza majengo muhimu ya kutolea huduma zote, katika kituo hicho cha afya.
ARUSHA DC
#kaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.