Serikali imewataka wenyeviti wa vijiji na mitaa kuhakikisha wanagawa viwanja vya kujenga kuanzia ukubwa wa mita za mraba 450 hadi 500 ili kurahisiha utoaji wa huduma kwenye nyumba hizo yanapotokea majanga ya moto.
Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Arusha Idrisa Kayembe kwenye kikao mafunzo juu ya ulioaji wa kodi ya ardhi, kilichowakutanisha wenyeviti wa vijiji na mitaa wa wilaya za Arumeru na Arusha kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi Creen Acres.
Kamishna huyo amesema kuwa, wenyeviti wa vijiji na mitaa, wanaowajibu wa kupanga miji katika maeneo yao kwa kuhakikisha wanapogawa viwanja katika maeneo yao, kugawa viwanja vyenye ukubwa wa kuanzia mita za mraba 450 mpaka 500 na si chini ya hapo.
Ameongeza kubwa ukubwa huo wa viwanja utaruhusu nafasi kati ya nyumba na nyumba, kwa ajili ya usalama wa nyumba hizo hasa wakati yanapotokea majanga ya moto pamoja na miundombinu ya maji taka, huduma ambazo zinakuwa ngumu kupatikana pale ambapo hakuna nafasi kati ya nyumba na nyumba.
"Tukiwa na nyumba zilizopangwa vizuri ni rahisi mamlaka za serikali kutoa huduma wakati wa majanga ya mto, majanga ambayo yanasababisha vifo na hasara kubwa kwa watu hasara ambazo zinaweza kuzilika kwa kupanga miji". Amesisitiza Kamishna Kayembe
Aidha amefafanua kuwa Wale watu wanaokata viwanja viwe na ukubwa unaoeleweka visiwe vidogo vidogo na vikikatwa vizingatie michoro ya mipango miji, lengo ni kuhakikisha wananchi wanakaa kwenye maeneo yaliyopangwa, maeneo yaliyopangwa ni rahisi kwa mamlka za serikali kutoa huduma wakati wa majanga ya moto na mengine.
Hata hivyo wenyeviti hao wamewaomba watalamu wa Ardhi na wengine kuhudhuria kwenye mikutano ya vijiji ili kutoa elimu ya namna bora ya mipango miji inayoendana na huduma zinazotakiwa kwenye makazi.
"Tunapofanya mikutano ya kujadili masuala ya ardhi, tunahitaji watalamu wa Ardhi, afya, maji, umeme, zima moto na wa mazingira ili waweze kueleimisha wananchi kufahamu taraibu za mamlaka zote, kwa kufanya hivyo tunaweza kupanga miji yetu bila kuchanganyana". Amefafanua Simon Siara Mwenyekiti wa mtaa wa Siara
ARUSHA
KaziInaendlea ✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.