• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Shilingi Bilioni 55.4 zapitishwa kwenye mpango wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha 2020/2021- Arusha DC

Posted on: January 30th, 2020

Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha, wamepitisha rasimu ya mapango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa makadirio ya mapato na matumizi ya kiasi cha shilingi bilioni 55.4, wakati wa mkutano maalum wa Baraza la Madiwaninuliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Akiwasilisha rasimu hiyo, kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Mchumi Albert Mahoo, amefafanua kuwa, kwa mwaka wa fedha 2020/2021, halmashauri  imepanga kukusanya na kutumi kiasi cha shilingi Bilioni 55.4, kutokana na ukomo wa bajeti uliotolewa na Hazina, kwa ajili ya bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020, kama inavyoelekezwa katika mwongozo wa maandalizi ya bajeti wa mwaka 2020/2021, ulioandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria na. 21 sura ya 439.

Ameeleza mchanganuo wa mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 55.4, ni pamoja na kiasi cha shilingi bilioni 4.9 kitatumika katika matumizi ya kawaida sawa na asilimia 8.86, shilingi bilioni 8.9 kitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo sawa na asilimia 16.8 huku shilingi bilioni 41.6 ikiwa ni ruzuku ya mishahara sawa na asilimia 75.06.

Katika kutekeleza miradi ya maendeleo, halmashauri itatumia mapato yake ya ndani kwa kiasi cha shilingi milioni 832.5, shilingi bilioni 3.5 fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na kuasi cha shilingi bilioni 4.5 ikiwa ni fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

Halmashauri imepanga kushirikiana na wananchi katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ili kufikia malengo ya dira ya taifa ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kuondoa umaskini.

Aidha amevitaja vipaumbele vya halmashauri hiyo kwa maka wa fedha 2020/2021 ninkatika sekta ya Elimu, Kilimo na Umwagiliaji,Mifugo na Uvuvi, Afya, aardhi, mipango Miji, Maliasili, Fefha na Biashara, Rasilimali Watu na Utawala, TEHAMA na maeneo mtambuka.

Hata hivyo wajumbe wa baraza hilo la madiwani, licha ya kupitisha mpango huo wa bajeti ili kuendelea na mchakato ngazi za juu, wamesema endapo bajeti hiyo itatekelezwa kwa ufanisi, itakuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa imepanga kutekeleza miradi inayowagusa wananchi moja kwa moja.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mhe. Baraka Simon, amesema kuwa ili mpango huo wa bajeti uweze kutekelezeka kwa ufanisi,  halmashauri inapaswa kubuni miradi ya kimkakati, miradi ambayo itailetea halmashauri  mapato na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa bajeti hiyo.

Ameongeza kuwa, licha ya  mpango wa bajeti kuwa na uhalisia lakini bado kuna changamoto ya utekelezaji wa miradi ya maji na miundombinu ya barabara, miradi ambayo imehamishiwa TARURA na RUWASA.

Naye Diwani wa Viti maalum, mhe. Jasmin Bachu, ameshauri kufanya tathmini ya wafanyabiashara ambao si waaminifu wenye vitambulisho vya wajasiriamali wakiwa na mitaji  mikubwa tofauti na tamko la mheshimiwa rais la kuwa na mtaji wa shilingi milini 4, jambo ambalo linakosesha halmashauri mapato na kodi nyingine za Serikali.

Halmashauri ya Arusha, imeweka mikajati ya ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo wa kielekroniki, kutoa elimu na kuhamasisha walipa kodi,ada na ushuru kwenye kata zote, kuboresha takwimu za walipa kodi, kuwa na mpango wa muda mrefu wa ushirikiano na sekta binafsi (PPP) katika uwekezaji mkubwa.




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.