Na. Elinipa Lupembe.
Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, shirika lisilo la Kiserikali la DSW limekabidhi samani za ofisi kwa ajili ya ofisi ya Dawati la Jinsia, kwenye kituo cha Polisi cha USA -River wilaya ya Arumeru.
Akizungumza wakati wa kukabidhi samani hizo za ofisi, ikiwemo viti, meza na viti vya wageni, Mkurugenzi wa Shirika la DSW, Peter Owaga, amesema kuwa, shirika limefikia uamuzi huo, mara baada ya kuona juhudi kubwa na kazi nzuri, zenye matokeo chanya kwa jamii, zinazofanywa na Serikali kupitia Dawati hilo kwa kushughulikia mashauri yanayohusu unyanyasaji wa kijinsia ndani ya wilaya ya Arumeru.
Aidha Owaga amefafanua kuwa, licha ya shirika hilo kutoa elimu na kuhamasisha jamii, juu ya ukatili wa kijinsia unaofanywa na jamii dhidi ya wanawake na watoto, lakini mafanikio makubwa yametokana na juhudi za Serikali katika kushughulikia kesi na mashauri ya ukatili wa kijinsia, shughuli zinazofanywa na Dawati la Jinsia kwenye vituo vya polisi nchini.
"DSW imepata matokeo na mafanikio makubwa kwenye miradi inayotekelezwa na shirika ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kutokana na juhudi na kazi kubwa inayofanywa na polisi kupitia Dawati la Kijinsia, matukio ya ukatili yameanza kupungua huku jamii ikanza kuhofia kutokana na sheria kutekelezwa kupitia Dawati la Jinsia" amesisitiza Mkurugenzi Owaga
Naye Msimamizi kituo cha Polisi Usa- River, Afande Juliana Maganga, licha ya kulishukuru shirika la DSW kwa msaada huo, ameweka wazi kuwa kwa sasa Jamii imeanza kutambua umuhimu wa haki za wanawake na watoto kutokana na serikali kuweka Dawati maalum la kushughulikia kesi na mashauri ya ukatili wa kijinsia unaofanyika kwenye jamii.
"Jamii inatambua kazi ya Dawati na tunapokea taarifa za matukio na kuyafanyia kazi kulingana na miongozo, taratibu na sheria, jambo ambalo linasababisha Jamii kuwa makini na kuanza kuogopa kufanya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuhofia kuingia kwenye migogoro ya kisheria na Jamhuri" amesisitiza Afande Juliana.
Hata hivyo Afande Juliana amekiri kuwa, kutokana na elimu na juhudi kubwa inayofanya na serikali kwa kushirikiana na Wadau, kwa sasa jamii kuanza kuwa na uwelewa wa pamoja juu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, jambo mabalo matukio yameanza kupungua tofauti na hapoa awali, lakini pia jamii inatoa taarifa pindi matukio yanapotokea.
Senorina Frank, Muelimisha Rika na Mwanafunzi wa darasa la VI, shule ya Msingi Olchoruvus kata ya Musa, amesema kuwa kupitia mradi wa Binti na Maendeleo, unaotekelezwa na shirika la DSW katika shule yao, wanafunzi wamepata ufahamu mkubwa juu ya ukatili waliokuwa wakifanyiwa na kutoka na mila na desturi ya jamii yao ya kimaasai, na kuongeza kuwa watoto wameanza kupinga ukatili huo kwa kuelimishana wao kwa wao pamoja na kuwaelemisha wazazi wao kuachana na mila hizo potofu.
"Kupitia Klabu yetu ya Binti na Maendelo shuleni, wanafunzi wengi tumepata ufahamu mkubwa, kwa sasa tunapinga ukatili wa kijinsia, wanafunzi wanajiamini na wanaona umuhimu wa kukataa kukeketwa, kukataa ndoa za utotoni kwa kuwaeleimisha wazazi wao kuachana na mila hizo potofu na wazazi wetu wameanza kuelewa sasa" amesema Senorina
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2022, yenye kauli mbiu ya "Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu" - Jitokeze zuhesabiwe, Shirika la DSW limefanya semina na makongamano mbalimbali, yaliyoshirikisha wadau wa maendeleo wakiwemo watoto, wanawake, Jeshi la Polisi, watalamu wa Serikali, waaathirika wa ukatili, waelimisha rika ngazi ya jamii na shule, walimi na wanafunzi, warsha iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shirika hilo eneo la Tengeru.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.