Shirika la eWater Tanzania limeanza kufanya majaribio ya mfumo wa kulipia maji kwa kutumia kadi ya kulipia kabla ya kutumia maji,kwa kutengeneza kituo cha kuchotea maji kinachotumia mfumo wa kielekroniki wa 'eWater- pay', katika eneo la stendi ya daladala ya Ngaramtoni.
Kituo hicho kimewekwa eneo hilo la stendi, maalumu kwa ajili ya majaribio ya matumizi ya teknolojia hiyo, na zaidi jamii ianze kuufahamu, kuutumia na kuuzoea, kabla ya kuanza kutumika rasmi.
Mratibu shirika la wa eWater -Arusha, Deogratius Nyusso, amesema kuwa kituo hicho cha kuchotea maji, kimewekwa kwa ajili ya majaribio ili kuwafanya wananchi waanze kuufahamu mfumo na kuuzoe kabla ya kuanza kutumika rasmi.
" Tumefunga mfumo kwenye kituo cha standi kama 'demo' watu waone na waanze kuifahamu teknolojia hiyo na kuitumia, zaidi kuwajenga kisaikolojia juu ya ujio wa teknolojia mpya ambayo hawajawahi kuitumia". Amesema Nyusso.
Ameongeza kuwa, matumizi ya teknolojia hiyo, yatasaidia kuthibiti upotevu wa rasilimali maji pamoja na uthibiti wa ukusanyaji wa mapato yanayotokana na malipo ya maji.
Godfrey Mollel mkazi wa Ngaramtoni, amethibitisha kuwa, endapo mfumo huo utatumika na kusimamiwa vizuri, unaweza kutatua changamoto ya udhibiti wa fedha za kuendesha miradi ya maji.
"Changamoto kubwa ya miradi yetu ya maji ni upotevu wa maji na mapato, kwa pamoja vinakwamisha maendeleo ya miradi ya maji, badala yake miradi hiyo hufa kwa kukosa fedha za matengenezo kutokana na usimamizi mbovu" amesema Mollel
Hata hivyo, teknolojia hiyo inategemea kutumika baada ya mradi wa maji wa vijiji vitano maarufu kama mradi wa maji wa WaterAid kukamilika, mradi unaotekelezwa na serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya nchini Uingereza 'DFID'.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.