Na Elinipa Lupembe
Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation For Tommorow (TFFT), linalofanya shughuli zake mkoani Arusha, limekabidhi darasa linaloongea kwa ajili ya wanafunzi wa darasa awali shule ya msingi Lemanyata, kata ya Lemanyata halamshauri ya Arusha.
Shirika hilo limekabidhi darasa hilo mara baada ya kulifanyia ukarabati na kulifanya kuwa darasa linaloongea (talking class) pamoja na samani zake, lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanajifunza kupitia milango yote mitano ya fahamu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi chumba hicho cha darasa na samani zake, Mkurugenzi wa shirika la TFFT ndugu Thabisani Ncubie, amesema mradi huo uliogharimu shilingi milioni 6.4, una lengo la kuwawezesha wanafunzi wa darasa la awali kupata ujuzi na maarifa kwa wepesi zaidi kupitia zana zilizopo katika darasa hilo.
Amesema kuwa, Shirika linaunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha mtoto wa darasa la awali anapata maarifa ya kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kabla ya kuingia darasa la kwanza.
"Tumeamua kuwezesha wanafunzi kufahamu KK tatu, yakiwa ndio malengo ya serikali ya awamu ya sita kwa wanafunzi wa elimu ya msingi, tunaamini darasa hili litakuwa nyenzo muhimu kwa watoto kujifunza kwa urahisi" Amefafanua Mkurugenzi Mcubie.
Hata hivyo akizindua darasa hilo Kaimu Mkurugenzi na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu, halmashauri ya Arusha Elizabeth Ngobei, amesema kuwa darasa hilo ni utekelezaji wa malengo ya serikali ya kuwa na mazinhira rafiki ya kufundishia na kujifunzia kupitia milango yote ya fahamu.
Serikali inatambua na kuthamini michango ya wadau ya kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu inayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa ufanisi na urahisi zaidi na kuwataka wadau kuendelea kusaidia kutatua changamoto za kijamii hususani kwenye sekta ya elimu.
"Kazi kubwa sasa iko kwenu walimu, kuwafundisha watoto hawa ili kugikia ndoto zao na malengo ya serikali lakini zaidi mnalo jukumu la kusimamia watoto kulitunza darasa na vifaa vyake ili vitumike kwa muda mrefu" Amebainisha Elizabeth
Naye Mwalimu wa darasa la awali mwl. Mwanaidi Mndeme amesema uwepo wa darasa hilo utamrahisishi kufundisha huku akiamini wanafunzi kuelewa kwa urahisi kupitia zana zinazohusisha milango yote ya fahamu.
"Mtoto anavutiwa zaidi kujifunza katika mazingira mazuri lakini zaidi kupitia zana kama hizi picha, vitu halisi pamoja na michezo, vifaa ambavo vipo darasani hapa". Amesisitiza Mwl.Mdeme
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya shuoe ya Msingi Lemanyata Philioo Ngaya, hakusita kushukuru na kuahidi kushirikiana na walimu kulitunza darasa hilo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Lemanyata Mwl. Elisaria Mmari, amesema kuwa shule ya hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,030, idadi inayosababisha upungufu wa vyumba madarasa shuleni hapo na kuwaomba wadau hao kuendelea kusaidia kutatua changamoto hiyo.
ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga'
KaziInaendelea ✍✍
Kaimu Mkurugenzi na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu, halmashauri ya Arusha Elizabeth Ngobei, akikata utepe kama ishara ya kuzindua Darasa Linalongea tayari kwa kunza kutumiwa na wanafunzi wa darasa la awali shule ya Msingi Lemanyata.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.