• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Shule ya Msingi Seliani wapata jengo jipya la choo cha kisasa, mara baada ya choo cha shule hiyo kutitia

Posted on: January 8th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Shirika lisilo la kiserikali la Kilimanjaro Technology, limekabidhi jengo la choo cha kisasa aina ya *SWASH* , chenye jumla ya matundu kumi, ujenzi uliogharimu jumla ya shilingi milioni 28, katika shule ya Msingi Seliani kata ya Kimnyaki, halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru.  

Shirika hilo linalofanya kazi zake Jijini Arusha na lenye makao yake makuu nchini Marekani, lilifikia uamuzi huo, mara baada ya choo cha shule hiyo kutitia mwezi Oktoba mwaka uliisha wa 2018 na kujeruhi mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza huku baadhi ya wanafunzi wakinusurika kuzama.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa jengo hilo la choo, mara baada ya kukamilika, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro, amewashukuru  wadau hao wa maendeleo kwa msada huo, msaada ambao umebeba thamani kubwa, kwa ustawi wa elimu ya watoto wa shule ya msingi Seliani na wilaya kwa ujumla.

Ameongeza kuwa choo ni muhimu sana kwa afya za wanafunzi wawapo shuleni,  na zaidi ni sehemu inayochochea tendo la kujifunza na kupandisha taaluma kwa wanafunzi, na kuwataka walimu kusimamia  wanafunzi wao, kukitunza choo hicho kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya choo hicho.  

Licha ya kuwapongeza wadau wanaojitokeza kuunga mkono juhudu za serikali ya awamu ya tano, Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wote kushiriki kuimarisha miundombinu ya shule zilizopo katika maeneo yao jambo ambalo litasaidia utoaji na upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wa taifa la Tanzania.

 "Kipekee niwashukuru sana shirika la Kilimanjaro Technology  na wadau wote kwa kutuunga mkono kwani moja ya kipaumbele cha serikali katika sekta ya elimu ni  uimarishaji wa ujenzi wa miundombinu kwa shule zetu zote, ili kuwezesha kuwa na mazingira bora ya kujifunza kwa wanafunzi" amesema mkuu huyo wa wilaya .

Akikabidhi msaada huo wa jengo la choo cha kisasa,  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,  Rais wa shirika la Kilimanjaro Technology, kutoka nchini Marekani, Bi. Laurel Werner amesema kuwa,  wameamua kutoa msaada huo kwa lengo la kuunga mkono kwa vitendo jitihada za serikali ya Tanzania, kuboresha Sekta ya Elimu ambayo imeanza kuonyesha mafanikio kupitia  Sera ya kutoa elimu bila malipo, kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

Bi. Laurel, amesema kuwa, serikali kutoa elimu bila malipo, inawapa nafasi na haki watoto wote kupata elimu hata wale wasio na uwezo,  hatua  ambayo imewavutia na kulazimika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe  Magufuli.  

Naye Lesasi Lukumai, mkazi wa Kimnyaki, wameushukuru uongozi wa shirika hilo na kuongeza kuwa ujenzi w choo hicho, umewapa wazazi amani na kuwa na uhakika wa usalama wa afya za watoto wao wawapo shuleni kwa kutumia choo imara,  bora na cha kisasa.

Hata hivyo mara baada ya uzinduzi wa jengo hilo, mkuu wa wilaya, amewaahidi wakazi wa eneo hilo kuwa, siku chachezijazo,  watazindua choo kingine cha kisasa chenye matundu 20, ambacho kimejengwa Kwa ushirikiano wa wananchi, serikali pamoja na wadau wengine wa Maendeleo,  ikiwa ni jitihada za kukabiliana na changamoto ya kutitia Kwa choo cha shule ya msingi Seliani na kujeruhi mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza.

Naye Afisa Elimu ufundi,halmashauri ya Arusha, Mwalimu Sokoine Mollel amesema kuwa, uwepo wa vyoo vya kisasa shuleni licha ya kuwa na faida kubwa  kiafya lakini pia huwezesha wanafunzi kurahisisha tendo la kujifunza na kufundisha na kufafanua kuwa jengo hilo la choo litatumiwa na watoto wa kike wa shule hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.