Na Elinipa J. Lupembe - ARUSHA
Inafahamika kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa la Tanzania, na takribani asilimia 80 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo hasa cha mazao ya chakuka na mbogamboga.
Halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa halmashauri nchini, ambayo wananchi wake hujishugulisha na kilimo na ufugaji, shughuli ambayo huitegemea kwa ajili ya pato la familia.
Kijiji cha Ilkiding'a, halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa vijiji, ambavyo wanachi wake wanajishughulisha na kilimo cha mbogamboga kupitia skimu za asili za umwagiliaji zilizoboreshwa na serikali.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi alipowatembelea wakulima hao kwenye mashamba yao, wameeleza kuwa, kupitia kilimo cha umwagiliaji wamepata mabadiliko katika uzalishaji wa mazao ya muda mfupi na mrefu pia, tofauti na awali walipokuwa wakitegemea kilimo cha majira ya mvua peke yake.
Juliana Tajiri, anazungumzia namna skimu za umwagiliaji zinavyowanufaisha kwa kuwawezesha kulima mazao ya mboga mboga, kwa kipindi cha mwaka mzima bila kutegemea msimu wa mvua, mazoa ambayo wamekiri kuwapatia chakula na kuongeza pato la familia kwa kuuza mazao hayo.
"Kupitia mifereji hii, tunalima mara tatu kwa mwaka, msimu wa kiangazi tunalima mara mbili mazao ya mbogamboga na msimu wa mvua tunalima mara mbili, mazao ya chakula huku uzalishaji wa mazao ya kudumu migomba na kahawa yakiendelea kutupatia kipato pia" ameseema Juliana.
Aidha wakulima hao wameishukuru serikali kwa kuzijenga skimu hizo za umwagiliaji kwa kuwa, ujenzi unazuia upotevu wa maji na kuwezesha kutumika katika shughuli za kilimo katika eneo kubwa na kuiomba serikali kusaidia kuendelea kuboresha mifereji hiyo ili kuzuia upotevu wa maji kwa baadhi ya maeneo.
Mkulima Jacob Mollel, amebainisha changamaoto ya upotevu wa maji, kwenye maeneo ambayo skimu za asili hazijajengewa na kuiomba serikali, kuendelea kuboresha mifereji katika maeneo yote ili wakulima hao wajikite zaidi kwenye kilimo hicho cha umwagiliaji, ambacho kimeleta mafanikio makubwa kwa wakulima, na kuthibitisha kuwepo na uhakika wa soko la mazao ya mbogamboga katika mkoa wa Arusha.
"Skimu hizi zimetuletea mafanikio makubwa sana, endapo mifereji yote itajengewa tutaondokana na upotevu wa maji na kwakuwa kiasi cha maji kinapungua siku hadi, kujengewa kwa mifereji kutazuia upotevu wa maji.
"Pamoja na faida tunayoipata kupitia mifereji hii, tunashirikiana na viongozi na wataalamu, kutunza mazingira ili Skimu hii ituwezeshe kulima mazao mengi zaidi na kuendelea kusaidia familia zetu”. Alisema Mariaki, mkulima wa zao la vitunguu.
Naye Afisa kilimo kata ya Ilkiding'a, Judith Maliya, amebainisha uwepo wa makampuni mbalimbali yanayouza madawa ya kuulia wadudu, madawa ambayo hayafahamiki madhara yake kwa mazao na kwa afya ya binadamu pia.
Hata hivyo Mhandisi wa mifereji halmashauri ya Arusha, Christaben Saria, amesema skimu hizo za asili zinasimamiwa na halmashauri kupitia Kamati za mifereji ambazo zinakatiba inayolelekeza utunzaji, ukarabati na uendelezaji wa skimu hizo.
ARUSHA DC
#KaziInaendelea
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA ZA MASHAMBA YA WAKULIMA KATA YA ILKIDING'A
Shamba la vitunguu
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.