TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI.
MAPOKEZI YA FEDHA MILIONI 110 ZA UKARABATI WA VITUO 5 VYA WALIMU.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, anautaarifu Umma kuwa, halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 110 kwa ajili ya ukarabati wa vituo 5 vya Walimu - Teacher's Resouces Cente (TRC), vituo ambavyo vilishapokea vifaa vya TEHAMA huku kila kituo kikigharimu kiasi cha shilingi milioni 22.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ikiwa ni fedha za utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa Elimu ya Msingi kwa Awamu ya pili (GPE - LANES II) Katika mradi huo wa vituo vitano, vituo vya walimu 2 vitajengwa upya kutokana na uchakavu wa majengo ambavyo ni Kituo cha walimu Ilkurot kata ya Lengijave na Kituo cha walimu Mlangarini kata ya Mlangarini huku vituo 3 vya Mringa kata ya Oloirien, Naurei kata ya Kiutu na Kambi ya Maziwa kata ya Mateves vitafanyiwa ukarabati.
Aidha Mkurugenzi Msumi amebainisha kuwa kulingana na maelekezo ya Serikali, mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha siku tisini kwa kutumia ‘Force Account' ukihusisha ujenzi na ukarabati wa majengo pamoja na ununuzi au utengenezaji wa samani za ndani viti na meza 45 kwa kila kituo.
Mradi huo unategemea kukamilika baada ya miezi 3 kuanzia sasa huku ikielekezwa mara baada ya kukamilika majengo na samani zote kupigwa chapa ya - GPE -LANES II.
#ARUSHA DC KaziInaendelea
Imetolewa na:
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.