Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, anautaarifu Umma kuwa Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 942.2 kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Miundombinu ya shule za Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya kutekeleza mradi mitatu ya maendeleo kwa Elimu Sekondari.
Mkurugenzi Msumi amefafanua kuwa katika kiasi hicho cha fedha, shiling milioni 584.2 zitumika kujenga shule mpya ya sekondari kata ya Moivo, shilingi milioni 260 ujenzi wa mabweni na ukarabati shule ya sekondari mringa na shiling milioni 98 ujenzi wa nyumba moja ya walimu yenye sehemu ya kuishi familia mbili (2 in 1) shule ya sekondari Kiutu.
Lengo la Serikali kutoa fedha hizo ni kuboresha miundombinu ya shule za sekondari ili kukuza kiwango cha elimu nchini na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira salama ikiwa ni pamoja na mazingira rafiki kwa walimu.
Aidha miradi hiyo itatekelezwa kwa kuzingatia taratibu na matumizi ya ’force Akaunti’ kwa muda wa miezi 3, huku shughuli za utekelezaji wa miradi hiyo, zikifanyika kwenye ngazi ya jamii kwa Usimamizi na Ushauri wa kitalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.