Kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019, halmashauri ya Arusha imefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.6 kupitia mapato ya ndani, ruzuku kutoka serikali kuu, wahisani pamoja na fedha za nje ya ukomo wa bajeti.
Katika taarifa ilyowasilishwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/19, miradi hiyo imetekelezwa kwa asiliami 60.6 ya fedha za bajeti ya shilingi bilioni 3.8 iliyopangiwa na Bunge, na asilimia 72 ya fedha nje za nje ya ukomo wa bajeti kiasi cha shilingi bilioni 2.8 na kufanya kutekeleza miradi kwa shilingi bilioni 6.6 .
Akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji ya Miradi ya Maendeleo, Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anastazia Tutuba amefafanua kuwa, kiasi cha shilingi bilioni 3.8 sawa na asilimia 60.69 ni fedha kutoka kwenye bajeti ya shilingi bilioni 6.4, zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo kisekta ikiwa ni Elimu, Afya, Maji, Mazingira, Kilimo na Ushirika, Mifugo, Ardhi, Fedha, Utawala na Mipango, fedha zilizotokana na Mapto ya Ndani, Serikali Kuu, wadau wa maendeleo na wahisani mbalimbali.
Ameongeza kuwa kiasi cha shilingi bilioni 2.0 kutoka kwenye bajeti ya shilingi bilioni 2.8 zilipokelewa kwa ajili ya Miradi ya jamii TASAF, miradi maji ya vijiji kumi (NWSSP), Miradi ya Elimu ya Lipa kulingana na matokeo (EP4R) pamoja na miradi ya maji ya Lipa kwa Matokeo (PBR).
Aidha taarifa hiyo imetoa picha halisi ya kasi ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya tano, na kushirikiana na wadau na wahisani, kutoa fedha za mirdi nje ya mpango wa bajeti zaidi ya shilingi bilioni mbili, fedha ambazo zimwezesha kufikisha maendeleo kwa wananchi wa hali ya chini katika vijiji vyote na kata zote.
Hata hivyo halmashauri imeweza kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia 80 kutoka vyanzo vyake vya ndani, mapato ambayo yametumika kuendesha halmashauri, kutoa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu, pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.