na Elinipa Lupembe
Diwani wa kata ya Bangata Mhe Ezra Tomito akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata ya Bangata kwa kipindi ya robo ya nne ya kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2023.
Mhe. Tomito ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu na afya, kuwezesha wananchi kiuchumi, pamoja na kuwawezesha wakulima wa mbogamboga katika kata hiyo.
Hata hivyo ameiomba serikali kuendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Bangata na kuzianisha changamoto hizo kuwa ni pamoja na uchakavu wa miundombinu ya shule zote za msingi za Bangata, Midawe na Sasi zinazohitaji ukarabati, ukosefu wa Kituo cha afya na ubovu wa miundombinu ya barabara
Awali Diwani huyo ameianisha mipango endelevu ya kata hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi ya Kata na vijiji, uboreshaji wa miundo mbinu ya maji kijiji cha Sasi na Bangata, ujenzi wa madarasa, upanuzi wa barabara za ndani, kusaidia vikundi vya kuweka na kukopa kuweza kupata mikopo ya bila riba inayotolewa na serikali katika kata sambamba na uboreshaji wa vivuko.
Mkutano huo umefanyika kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmasahuri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.