Na Elinipa Lupembe
Kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 cha kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2022, Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji (TARURA) wilaya ya Arumeru, imefanya matengenezo ya kawaida barabara za halmashauri ya Arusha zenye urefu wa Kilomita 24.8.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kipindi cha robonya pili, mkutano wa Baraza la Madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, kwa niaba ya Meneja wa TARURA Arumeru, Frank Mwanga, barabara hizo zenye urefu wa Km 24.8 zimetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 931.7 zikiwa ni fedha za Tozo.
Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimejumuisha matengenezo ya kawaida ikiwa ni pamoja na kuchonga barabara hizo, kuweka changarawe, ukarabati wa kuta za madaraja na ujenzi wa makaravati na vivuko kwa baadi ya barabara pamoja na mitaro ya kutolea maji.
Awali huu ni utekelezaji wa Ilani ya CCM iliyolenga kuboresha miundombinu ya barabara, ili kuwezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tuungane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.