Na. Elinipa Lupembe.
Umoja wa Wakuu wa shule za sekondari ' Tanzania Head of Secondary Schools Association -TAHOSA, halmashauri ya Arusha, wamekabidhi vifaa vya ujenzi kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za halmashauri yao, katika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.
Wakuu hao wa shule, kupitia umoja huo wa TAHOSA, wametoa vifaa vya ujenzi, ikiwemo mabati 50 na mifuko 30 ya saruji, yenye thamani ya shilingi milioni 2.1, lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, katika shule za sekondari za halmashauri ya Arusha, wanaojiunga na masomo hayo ya sekondari.
Akizungumza wakati wa kukabidhi, vifaa hivyo vya ujenzi, mwenyekiti wa TAHOSA Halmashauri ya Arusha, mwalimu Dr. Ivan Mmari, amesema kuwa, lengo la kutoa vifaa hinyo ni kuunga mkono juhudi za halmashauri hiyo, za ujenzi wa vyumba vya madarasa, na kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, wanakwenda shule na kuendelea na masomo yao katika mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.
"Sisi kama walimu, wenye jukumu la kusimamia shule, tumeguswa na kazi nzuri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika shule zetu, tukaona ni vema na sisi tukaungana na serikali, wadau na wanachi wanaojenga vyumba hivyo vya madarasa, sisi kama walimu hatujisikii vizuri watoto waliofaulu vizuri kukosa darasa la kusomea, au kubanana katika chumba kimmba cha dasara, tunawahurumia sana, kwa kuwa tunaamini mazinhira bora ya kujifunzia na kufundishia yanaleta matokeo mazuri kielimu" amesema Dr. Mmari
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Bangata, mwalimu Grace Minja, amesema kuwa kama walimu wameguswa sana na jitihada za ujenzi wa miundombinu wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika shule za sekondari wanazoziongoza, nakuona ni vema kutoa chochote ili kuungana na wadau wengine, kumuunga mkono mkurugenzi mtendaji wa halmashauri yao, ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa unaonedelea.
Akizungumza wakatiokea vifaa hivyo, mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, amewashukuru wakuu hao wa shule, kwa kuguswa na changamoto hiyo ya upunhufu wa vyumba vya madarasa na kuchangia mabati na saruji, ili kuongeza nguvu za kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri, na kuongeza kuwa vifaa hivyo vya ujenzi, vimekuja wakati muafaka kutoakana na uhitaji wa mabati na saruji za umaliziaji wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya sekondari Bangata, Kimnyaki na Mringa ili kukamilisha vyumba 35 kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Februari 2021.
" Niwashukuru TAHOSA, mmefanya jambo jema sana, licha ya kuwa halmashauri ilikuwa na upungufu wa vyumba 35 vya madarasa, sisi tumeanzisha ujenzi wa vyumba 52, kukamilika kwa vyumba hivyo,kutakuwa na ziada ya vyumba 17, lengo hasa ni maandalizi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka ujao wa 2022" amefafanua Mkurugenzi Mtambule.
Hata hivyo, Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, mwalimu Medard Lupenza, atoa takwimu za wanafunzi waliofaulu katikanhalamshauri ya Arusha na kusema kuwa, jumla la wanafunzi 7,691 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, kutokana na upungufu wa vyumba 35, jumla wa wanafunzi 1133, wanategemea kuchaguliwa kwa awamu ya pili ' second selection', hata hivyo mpaka kufikia tarehe 28.Februari 2021, wanafunzi wote watakuwa wameanza shule, hasa kwa kuzingatia agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu, mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Aidha mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, amewashukuru wananchi na wadau wote wa maendeleo walioshiriki katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na nawakaribisha wadau wote wa maendeleo katika sekta ya elimu ndani nna nje ya nchi, kujitokeza kuchangia, vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya shule, vifaa vya kujifunzia na kufundishia ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazinhira bora yanayochangia maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu.
PICHA ZA MATUKIO YA MAKABIDHIANO YA MABATI
Wawakilishi wa Umoja wa wakuu wa shule za Sekondari -TAHOSA, wakimkabidhi mabati 50, mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha! Saad Mtambule (wa kwanza kulia), kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya makao makuu ya halamahauri hiyo eneo al Sekei.
Mkurugenzi Mtendaji halmshauri ya Arusha, akizungumza na wawakili wa wakuu wa shule za sekondari- TAHOSA, mara baada ya kupokea vifaa vya ujenzi, eneo la makao makuu ya halamshauri ya Arusha.
Picha ya pamoja ya wawakilishi wa umoja wa wakuu wa shule za sekondari - TAHOSA na mkurugenzi Mtendajindaji, Halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule ( wa tatu kutoka kulia).
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.