Halmashauri ya Arusha inategemea kufanya Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani (Full Council) wa robo ya pili mwaka wa fedha 2020/2021, kwa kipindi cha kuanzia Oktoba mpaka Desemba 2020. Mkutano huo utakaofanyika tarehe 29.01.2021 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:00 asubuhi.
Mkutano huo wa baraza la Madiwani utakuwa na ajenda 10, huku agenda kuu zikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, Kujadili taarifa ya Mapato na Matumizi, Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Kupitisha Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Uhamasishaji wa Maendeleo ya Jimbo, Kuteua Madiwani wawakilishi wa Baraza La Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni, pamoja na kujadili Masuala ya kiutumishi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa. Mkutano Baraza la Madiwani ni Mkutano wa wazi, hivyo wananchi wote wa Halmashauri ya Arusha wanatakiwa kuhudhuria, ili kufuatilia kwa uwazi shughuli za utekelezaji wa Maendeleo zilizotekelezwa katika Halmashauri yao kwa kipindi cha miezi mitatu na robo ya pili, mwaka wa fedha 2020/2021.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.