TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA NA POSTIKODI.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, anawatangazia Watanzania wote wenye sifa zinazohitajika na wenye nia yya kufanya kazi ya zoezi la Anwani za Makazi katika Kata na Vijiji vya Halmashauri ya Arusha, kuomba nafasi hizo.
A: SIFA ZA MWAOMBAJI
1. Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 -35
2. Awe amemaliza Kidato cha 4 na kuendelea
3. Awe anajua Kusoma na Kuandika
4. Awe anamiliki simu Janja yenye sifa ya Android 7 na uwezo wa kukaa na chaji kwa siku nzima
5. Awe na Uwezo wa kutumia simu Janja6. Awe na Akili timamu.7. Awe na barua pepe ( email) na nywila (password) inayofanya kazi.
B: KAZI NA MAJUKUMU:-
1. Kugawa /Kuandika namba za nyumba, viwanja na maeneo ya huduma
2. Kukusanya taarifa za nyumba, Viwanja na maeneo ya huduma
3. Kukusanya taarifa za wamiliki wa nyumba na maeneo ya huduma kwa kutumia Mfumo wa Anwani za Makazi.
4. Kutuma Data kwenye Mfumo wa Anwani za Makazi
C: MAOMBI YAAMBATANISHWE NA :-
1. Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne na cheti cha taaluma.
2. Nakala ya cheti cha Kuzaliwa3. Picha ( passpory size 2)
3. Kwenye barua ya maombi, Mwombaji aandike namba zake za simu zinazopatikana.
D: MALIPO:-
1. Malipo ya Ajira ya muda ni Tsh. 10,000/= kwa siku
E: JINSI YA KUTUMA MAOMBI:-
1. Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono zikiwa na Anwani kamili ya mwombaji.
2. Barua ya maombi ipitishwe kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji husika na kuiwasilisha barua hiyo kwa Afisa Mtendaji wa Kata husika.
.3. Mwombaji anashauriwa kuomba nafasi kwenye Kata anayoishi
F:MAOMBI YOTE YATUMWE KWA ANWANI IFUATAYO:-
Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Arusha,
S.L. P 2330,
ARUSHA.
G: TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI:-
Mwisho wa kupokea yote maombi ni tarehe 24.02.2022 saa 09:30 Alasiri.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.