Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo anategemea Kuzindua Kampeni ya Chanjo ya Ugonjwa wa Polio na Surua -Rubela kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 mpaka miaka 5.
Uzindizi huo utafanyika kwenye Kituo cha Afya Nduruma, kata ya Nduruma, Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru kuanzia saa 03:00 asubuhi.
Baada ya uzinduzi, huduma hiyo ya Chanjo itaendelewa kutolewa kwa muda wa siku saba kuanzia kesho tarehe 17-21/10/2019 kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya (vya Serikali na Binafsi). Ewe mzazi au mlezi mwenye mtoto wa umri huo, hakikisha unampeleka mwanao kupata chanjo hizo muhimu, kwenye kituo kilicho jirani nawe.
Huduma itatolewa kuanzia saa02:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.
*CHANJO NI BORA KULIKO TIBA* *MPENDE MWANAO JALI AFYA YAKE*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.