Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la ARUMERU MAGHARIBI, kwa kuzingatia Kanuni ya 14 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka wa 2020 na kanuni ya 12 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2020. Anakaribisha Maombi kwa Watanzania wenye Sifa na uwezo wa kujaza nafasi za Watendaji wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28.Oktoba, 2020 kama ifuatavyo:-
1. MSIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA (Nafasi 629)
2.WASIMAMIZI WASAIDIZI WA KITUO CHA KUOIGIA KURA (Nafasi 629)
3. KARANI MWANGOZA WAPIGA KURA (Nafasi 629)
SIFA ZA MWOMBAJI KWA NAFASI YA MSIMAMIZI WA KITUO/WASIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA:-
I. Awe Raia wa Tanzania mwenyee umri wa miaka 18 au zaidi.
II. Asiwe shabiki au Kiongozi wa Chama Cha Siasa.
III. Awe mwadilifu elimu ya Kidato cha 4 au zaidi na anayeweza kusoma na kuandika vizuri. Pia anayeweza kuyaelewa maelekezo ya wasimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura.
IV. Ikiwezekana awe Mkazi wa Kata ambayo anaomba.
1. SIFA ZA MWAOMBAJI KWA NAFASI YA KARANI MWANGOZA WAPIGA KURA.
I. Awe Raia wa Tanzania mwenyee umri wa miaka 18 au zaidi.
II. Awe Mkazi wa Kata ambayo atafanyakazi ya Kuongoza WAPIGA KURA.
Asiwe shabiki au Kiongozi wa Chama Cha Siasa.
III. Ikiwezekana awe Mpiga Kura wa Kituo anachofanya Kazi.
IV. Awe mwadilifu
Na mwenye Akili Timamu.
V. Awe na Elimu isiyopungua Kidato cha 4 na anayeweza kusoma na kuandika na kuyaelewa maelekezo ya Wasimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura.
IV. Asiwe shabiki au Kiongozi wa Chama Cha Siasa.
**MALIPO**
i.Malipo yatakuwa kama ifuatavyo:-
Msimamizi wa Kituo siku ya Uchaguzi atalipwa posho ya Tzs. 35,000 kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Tzs 15,000 kwa siku moja na nauli Tzs 20,000;
ii. Msimamizi Msaidizi wa Kituo atalipwa posho ya Tzs. 30,000 kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Tzs 15,000 na nauli Tzs 20,000; na
iii.Karani Mwongozaji Wapiga Kura atalipwa posho ya Tzs 30,000 kwa siku moja na posho ya chakula Tzs 15,000.
**MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE**
i. Waombaji waambatishe maelezo binafsi (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wawili.
ii. Maombi yote yaambatane na Vyeti vya taaluma, nakala za Vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita au kuhitimu mafunzo kwa kuzingatia sifa kwa mujibu wa Tangazo hili.
iii. Waombaji waambatishe picha mbili Passport size za hivi karibuni.
iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao.
iv.Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kugushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 27 Septemba , 2020.
Anuani ya kutuma maombi ya kazi ni:-
Msimamizi wa Uchaguzi,
Jimbo la Arumeru Magharibi
S.L.P. 2330
ARUSHA.
----------------------
Saad A. Mtambule
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.