Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote kuwa, kesho tarehe 09.11.2018 kutakuwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasilsiha taarifa za Kata kwa kipindi cha robo ya kwanza, cha kuanzia mwezi Julai mpaka Septemba, 2018, mkutano utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Mkuatano huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa, ambao unatoa fursa kwa Waheshimiwa Madiwani kuwasilisha taarifa za kata zao.
Taarifa hizo, zinajumuisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na mipango endelevu ya kata husika.
Mkutano huo wa Baraza la kata utakuwa na ajenda 6 huku agenda kuu ikiwa ni kuwasilisha taarifa za kata zote 27 za halmashauri ya wilaya ya Arusha.
Aidha Mkurugenzi Mahera, anawataka wananchi wote wa Halmashauri ya Arusha Kuhudhuria Mkutano huo unaojadili Maendeleo ya Halmashauri yao kwa ujumla wake.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.