Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa zinazohitajika na wenye nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuomba kujaza nafasi wazi za kazi kupitia kibali Kumb.Na. FA.170/371/01/104 cha tarehe 30 April ,2020 kilichoidhinisha nafasi mbalimbali za kazi kama ifuatavyo:
KATIBU MAHSUSI DARAJA III ( NAFASI 2)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu.
Awe amefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.
Awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika progam za Windows, Microsoft Office, Excel, Internet, Email na Publisher.
1.2 NGAZI YA MSHAHARA
Cheo cha Katibu Mahsusi Daraja III kina ngazi ya mshahara wa TGS B1.
.1Kazi na majukumu ya Katibu Mahsusi Daraja III
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
Kusaidia kupokea wageni na kuwasiili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
Kusaidia kutunza taarifa/ kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka, au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
Kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.
MSAIDIZI WA KUMBUKUMU DARAJA II ( NAFASI 2)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe amehitimu kidato cha IV au VI
Awe ametunukiwa cheti (NTA Level 5) cha utunzaji kumbukumbu katika moja ya fani za Afya, Masijala, Mahakama na Ardhi.
NGAZI YA MSHAHARA
Cheo cha Katibu Mahsusi Daraja III kina ngazi ya mshahara wa TGS B1.
2.3 KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMU DARAJA III
Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka / mafaili yanayohitajika na wasomaji.
Kudhibiti upokeaji , uandikishaji wa kumbukumbu / nyaraka.
Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu,nyaraka katika makundi kulingana na somo husika ( classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Kuweka/ kupanga kumbukumbu/ nyaraka katika reki (file racks / cabinets) katika masijala/ vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
Kuweka kumbukumbu (barua / nyaraka n.k) katika mafaili.
Kushughulikia maombi ya kumbukumbu / nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
3. MASHARTI YA JUMLA KWA NAFASI ZOTE
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.
Waombaji waambatanishe wasifu (C.V) wenye anuani sahihi, namba za simu sahihi, pamoja na majina matatu ya wadhamini na namba za simu zinazopatikana.
Testimonial “provisional Result” Statement of Result, hati ya matokeo ya kidato cha nne/Sita HAVIKUBALIKI.
Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na TCU au NECTA.
Watumishi waliostaafishwa kazi Serikalini kwa namna moja au nyingine hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha mamlaka stahiki.
Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo:
Cheti cha kuzaliwa
Cheti cha kuhitimu elimu ya Kidato cha nne (IV) na Sita (VI) kwa wale waliofika kiwango hicho.
Cheti cha taaluma na mafunzo mbalimbali.
Passport size 1
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10/06/2020
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili “HAYATAFIKIRIWA”.
MAOMBI YOTE YATUMWE KWA NJIA YA POSTA KATIKA ANUANI IFUATAYO:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA,
S.L.P 2330,
ARUSHA.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.