*TANZIA*
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Idara ya Elimu Sekondari na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mlangarini, Dkt. Mwl. Elisa Pallangyo, kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 09.03.2021 katika Hospitali ya Serian alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mkurugenzi Mtambule, ametoa pole kwa familia ya Daktari, Mwalimu Pallangyo, ndugu, jamaa, marafiki, walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mlangarini, Idara ya Elimu Sekondari pamoja na watumishi wote halmashauri ya Arusha.Mazishi yanategemea kufanyika kesho tarehe 13.03.2021 nyumbani kwao Ngarenanyuki, wakati huo huo Ibada ya kuaga mwili wa marehemu inafanyika leo tarehe 12.03.2021 kuanzia saaa 06:00 mchana katika viwanja vya shule ya Sekondari Mlangarini.
Watumishi wote wa Halmashauri ya Arusha wanaungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki, katika kuoboleza msiba wa Dkt, Mwl. ELISA PALLANGYO.
Tangulia Daktari, tangulia Mwalimu, tangulia mpendwa wetu. VITA UMEVIPIGA, KAZI UMEMALIZA.
Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu Dkt. Mwl. Elisa Pallangyo mahala pema peponi.
Rest in peace Dr.Pallangyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.