Na Elinipa Lupembe
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ufadhili wa shirika la watoto Duniani (UNICEF) wametoa vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi kwa wasichana 12, 943 wanaotoka kwenye kaya zilizo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi taulo hizo, kwa wasichana wa kata ya Kiutu, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi ameishukuru serikali kupitia TASAF kwa kutoa vifaa hivyo ikiwemo taulo za kike, vifaa ambavyo vinawahakikishia watoto kuwa na hedhi salama isiyo na vikwazo.
Ameongeza kuwa vifaa hivi ni mkakati wa serikali wa kuhakikisha mazingira bora ya wanafunzi kupata elimu bila kikwazo na kuhakikisha watoto wote wanahudhuria masomo pasi kuwa na tatizo la kiafya hususa kipindi cha hedhi.
"Serikali inahakikisha kila mwanafunzi anahudhuria masomo mwaka mzima, bila kuwa na vikwazo, hivyo tunzeni viafaa hivyo, kwa kuhakikisha vinawasidia, bila
Hata hivyo wanafunzi hao, wamemshukuru mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu kupitia TASAF kwa masaada huo, ambao wamebainisha kuwa ni kiwafanya watoto wa kaya masikini kupata mahitaji sawa na watoto wengine.
Catherini Felix msichana aliyehitimu kidato cha IV mwak huu 2022 shule ya sekondafi SOKON II, baadhi ya wazazi wamekuwa wakishindwa kumudu kuwanunulia watoto wao wa kike, vifaa salama wakati wa hedhi kutokana na uwezo wa kifedha kuwa mdogo, lakini serikali imekuja kuwasaidia wasichana wengi kutoka famili zisizo na uwezo mkubwa kifedha.
Baadhi ya wasichana hushindwa kuja shuleni wkati wa hedhi kutokana na kukosa taulo za kike, na kuwafanya kushindwa kufanya vizuri kitaaluma sawa na wavulana" .Amefafanua Lightnes Maina msichana aliyehitimu kidato cha IV mwaka huu Sekondari Sokon II.
Awali Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amethitisha kupokea vifaa vya wasichana 12, 943 kwa ajili ya wasichana walio kwenye kaya 12, 288 zinazonufaika na Mpango wa Kunusuru kaya Maskini kwenye vijiji 88 vya halmasahuri hiyo.
Ifahamike kuwa Miradi ya serikali inayotekelzwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia Serikali kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika kukabiliana na changamoto za umasikini kwa wwananchi nchini
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.