• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DKT. KIWONE: TEKNOLOJIA YA UHIMILISHAJI NG'OMBE WA MAZIWA MKOMBOZI WA MFUGAJI

Posted on: August 8th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.   

     Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa, wametakiwa kubadili mtazamo na kuanza kufuga kibiashara kwa tumia teknolojia ya kisasa ya Uhimilishaji, teknolojia ambayo ni mkombozi na imeleta mapinduzi makubwa kwa wafugaji wengi kwa kufuga ng'ombe bora wa maziwa, wenye kuongeza pato la mfugaji.

     Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,  kwenye viwanja vya maonesho ya Wakulima Kanda ya Kaskazini, ndani ya Banda la Mifugo, halmashauri ya Arusha, Daktari wa Mifugo halmashauri hiyo, Dkt. Yohana Kiwone, ameanza kwa kueleza kuwa, ili wafugaji waweze kujikomboa kiuchunmi wanatákiwa kufuga kisasa, ufugaji utakaowaongezea kipato, ni vema kutumia teknolojia ya uhimilishaji, teknolojia inayomuwezesha mfugaji kuchagua mbegu bora ya ng'ombe, ng'ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa mengi, nyama nyingi na ngozi bora kwa biashara na viwanda.

     Amefafanua kuwa teknolojia ya uhimilishaji, ni teknolojia inayoruhusu ng'ombe kumpandikizwa bila dume, na kupata mbegu bora ya ng'ombe, mwenye uwezo wa kutoa lita 20 mpaka 30 za maziwa kwa siku, na kumuwezesha mfugaji kuchagua aina ya ng'ombe anayemtaka na jinsia ya ng'ombe anayotaka.

      Hata hivyo ameweka wazi kuwa teknolojia ya uhimilishaji, imeleta mapinduzi makubwa katika uzalishaji wa maziwa hasa kwa wafugaji wanaofugia ng'ombe ndani, wengi wamepata mafanikio makubwa  kwa kubadili uzao wa ng'ombe wao, na ng'ombe hao kuzaa ng'ombe bora wenye kutoa maziwa mengi, jambo ambalo limewaongezea kipato kwa sasa, tofauti na hapo awali.

     "Kuelekea uchumi wa viwanda, mfugaji anatakiwa kuachana na kufuga kienyeji, badala yake afuge kisasa, mifugo itakayotoa mazao  yenye ubora kwa matumizi ya viwanda, teknolojia ya uhimilishaji pekee, ndio teknolojia inayoweza kumfanya mfugaji kupata rasilimali za kuweza kuendesha viwanda vinavyotengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa" amesisitiza Dkt. Kiwone.

     Aidha amefafanua kuwa, endapo mfugaji atakuwa na ng'ombe bora anayetoa wastani wa lita 20 kwa siku, anauwezo wa kupata shilingi elfu 20 kwa siku, na shilingi laki 6 kwa mwezi, huku akiwa na uhakika wa kupata nyama na ngozi bora pindi ng'ombe huyo atakapofikisha umri mkubwa wa kukoma kuzaa.

   "Kiasi cha shilingi laki 6 kwa mwezi ni kisio la chini kwa mfugaji anayenza na ng'ombe mmoja, lakini mfugaji akiwa na ng'ombe watano anaweza kupata shilingi laki 1 kwa siku, kwa mwezi ni shilingi milioni 3 na kwa mwaka ni milioni 36, biadhara ambayo itamkomboa mfugaji na kuimarisha uchumi wake binafsi na uchumi wa Taifa.

    Kwa sasa wafugaji wa ng'ombe Halmashauri ya Arusha, waliotumia teknolojia ya uhimilishaji wameanza kuona na mafanikio ya teknolojia hiyo, kumwkuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji kwa mwaka 2019/2020 jumla ya ng'ombe 3,538 wamezaliwa ikiwa ni wastani wa ng'ombe 295 kwa mwezi.

     Teknolojia hiyo ya uhimilishaji inapatikana kwenye viwanja vya maonesho ya wakulima Njieo, fika kwenyw Banda la mifugo halmashauri ya Arusha, na baada ya maonesho fika ofisi za Mifugo halmashauri ya Arusha eneonla Sekei, utapata huduma hiyo, shime wafugaji tuchangamkie fursa hiyo. 

                          'Tanzania ya Viwanda iko mikononi mwetu'.


"KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI, CHAGUA VIONGOZI BORA 2020" 


PICHA ZA BANDA LA MIFUGO ARUSHA DC

Daktari wa Mifugo halmashauri ya Arusha, Dkt. Yohana Kiwone akimuelezea ng'ombe aliyezaliwa kwa teknojia ya Uhimilishaji, ng'ombe ambaye anatoa lita 20 za maziwa kwa siku akiwa tayari ana mimba ya miezi 3.


Ng'ombe waliozaliwa kupitia teknolojia ya Uhimilishaji, wakiwa kwenye Banda la Mifugo halmashauri ya Arusha kwenye maonesho ya wakulima Kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi- Njiro Jijini Arusha.

Ng'ombe bora wa maziwa mwenye uzito mkubwa na mwenye uwezo wa kutoa maziwa lita 20 mpaka 30 kwa siku.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.