Na. Elinipa Lupembe.
Timu maalum ya ufuatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, imeridhishwa na utekelezaji wa mradi ya maendelea hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa, halmashauri ya Arusha, ujenzi unaotekelezwa kupitia fedha za Mpango wa Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Akizungumza kwa niaba ya timu hiyo, wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mkurugenzi wa OR- TAMISEMI, Idara ya Afya Dr. Ntuli Kapologwe, ameweka wazi kuridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri ya Arusha, mara baada ya kupitia na kukagua jumla ya miradi 5, miradi 4 ya ujenzi wa madarasa na mradi mmoja wa upanuzi wa kituo cha Afya Oldonyosambu.
Hata hivyo Dr. Kapolongwe amepongeza ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa wakati, huku madarasa hayo yakiwa na ubora unaolingana na thamani ya fedha ziliotolewa na serikali za kukamilisha ujenzi huo.
"Niwapongeze kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati, lakini niwapongeze kwa ubora wa madarasa unaozingatia thamani ya pesa, madarasa yamejengwa kwa ubora, yamewekwa 'tiles', tofauti na maeneo mengine, wengi wameweka sakafu ya saruji, lakini pia kila darasa lina meza na viti 50, kuna miundombinu ya watu wenye ulemavu, huku baadhi ya shule zimejengwa na ofisi za walimu, hii inaonyesha kuwajali walimu, zaidi nimeshuhudia namna watumishi mlivyojipanga, inaonesha wazi mnafanya kazi kama timu, hongereni sana Arusha DC" amesisitiza Dr. Kapolongwe
Aidha, Dr. Kapolongwe amemuagiza mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, kusimamia ukamilishaji wa madarsa katika shule mbili zinazojenga majengo ya ghorofa pamoja na kuwa na mkakati wa ujenzi wa ofisi za walimu wakati wa ujenzi wa miundombinu ya shule, lengo likiwa ni kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi na mazingira rafiki ya kwa walimu pamoja na miundo mbinu ya walemavu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameishukuru serikali kupitia timu hiyo maalum kwa kutembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya ujezi wa vyumba vya madarasa na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na timu hiyo, na hatimaye kufikia adhma ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wote, waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2022, wanaanza masomo yao kwa wakati.
Awali timu hiyo maalumu ya ufuatiliaji kutoka TAMISEMI, wametembelea jumla ya miradi 4 ya elimu na kupitia jumla ya vyumba 27 vya madarasa katika shule 4, ujenzi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 540 fedha za Mapamabano dhidi ya UVIKO 19 na mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Oldonyosambu, mradi utakaogharimu kiasi cha shilingi 500.
Ikumbukwe kuwa, halmashauri ya Arusha ilipokea fedha za ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa, mradi utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2, fedha za mkopo wa riba nafuu kutoka benki ya Dunia, ikiwa ni fedha za Mpango wa Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19.ARUSHA DC#Kaziiendelee ✍✍
Timu ikikagua ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa shule ya sekondari Mringa
Timu ikikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya sekondari Mukulat
Timu ikikagua ujenzi wa vyumba 13 vya madarasa shule ya sekondari Kiranyi
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.