Afisa Maendeleo ya Jamii ndugu Getrude Darema ameongoza timu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na watumishi wa kata za Olkokola na Oldonyowasi kuwaelimisha wananchi wa rika zote kwenye soko la Oldonyosambu na kutoa elimu ya kuachana na kilimo, biashara pamoja na matumizi ya bangi na pombe haramu ya gongo.
Darema amewataka vijana waliokuwa katika soko la Oldonyosambu kuchana kabisa na matumizi ya bangi na pombe haramu ya gongo kwani ni kinyume cha sheria na zaidi inawaathiri vijana hao kiafya na kuwa na vijana wasio na uwezo wa kufanya kazi kabisa na kuwasisitiza vijana kuachana na kupiga vita ndoa za utotoni na ukeketawaji wa watoto wa kike kwani vijana ndio nguzo ya mabadiliko katika jamii yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.