Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha, imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri ya Arusha.
Kiongozi wa timu hiyo Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Moses Mabula amesema kuwa ukaguzi wanaofanya ni shughuli za kawaida za ofisi ya mkuu wa mkoa za kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa kwenye halmashauri zote za mkoa wa Arusha.
Mabula ameelezea malengo hasa ya ukaguzi wa miradi unaofanywa na mkoa, kwenye halmashauri zake:-
# Kuoanisha uhalisia wa miradi ile iliyoidhinishwa kwenye bajeti ndio inatekelezwa na kuweza kufanya mapitio ya bajeti.
# Kujionea hali halisi ya miradi kama inaendana na thamani halisi ya fedha iliyotumika kutekeleza miradi hiyo 'value for money'.
# Kuona kama malengo ya mradi yaliyokusudiwa kama yametimia na yanaendana na uhitaji wa wananchi na jamii ya eneo husika.
# Kuona namna ya ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao na kufanya tathmini matumizi ya 'Forced Account' kwa kulinganisha na miradi inayotumia wakandarasi.
# Kujiridhisha na uchangiaji wa asilimia 60% ya mapato ya ndani ya halmashauri kwenye shughuli za zmaendeleo pamoja na kutoa ushauri kwa ajili ya maboresho.
# Kuona endapo halmashauri inatenga na kuto 10% ya mapato yake ya ndani kwa vikundi vya wanawake na vijana kwa kutembelea vikundi vilivyopata mkopo huo, kuona shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo pamoja na kufanya tathmini ya mikopo hiyo.
# Kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
# Kufanya tathmini kwa ajili ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi kwa bajeti ijayo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.