Na. Elinipa Lupembe.
Timu ya watalamu wawezeshaji ngazi ya Halmashauri wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, unaotekelezwa TASAF III, awamu ya pili, wametakiwa kwenda kufanyakazi kwa uadilifu huku wakiweka uzalendo na waaminifu mbelr katika zoezi la uhakiki wa walengwa, zoezi litakalofanyika katika vijiji vyote vya halmshauri ya Arusha wilaya ya Arumeru.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msimamizi wa Ufuatiliaji na Tathmini TASAF, Makao Makuu, Farid Mishaeli, alipokuwa akifungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo timu hiyo ya watalamu wawezeshaji, ngazi ya halmashauri, mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Arusha.
"Kila mtaalamu anatakiwa kufanyakazi kwa weledi na uaminifu mkubwa katika uhakiki, ili kupata kaya zenye sifa halisi za umaskini zilizoainishwa na mradi kuingia kwenye mpango, kwa lengo la kufikia adhma ya serikali ya kuzikwamua kaya hizo.
Amesema kuwa zoezi hili linafanyika kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais, wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya uhakiki nchi nzima ili kuondoa kaya zilizopoteza sifa kwa namna moja au nyingine na kuziingiza kaya zenye vigezo halisi vilivyoainisha.
Aidha Mishael amefafanua kuwa, lengo la serikali ni kuondoa umaskini nchini kwa kuwawezesha walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika kukuza kipato kwa kujikita kwenye uzalishaji sekta ya kilimo, ufugaji na biashara ndogondogo.
Naye Kaim Mkurugenzi, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, amethibitisha kuwa, menejiment imeteua watalamu wenye sifa kwa kuzingatia vigezo na weledi wa kufanyakazi hiyo, na kuahidi kusimamia zoezi hilo kuafanyika kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia vigezo vyote vilioainishwa kisheria.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo, amewataka watalamu hao, kuzingatia mafunzo watakayoyapa, ili kuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuhakikisha kaya zote zenye sifa zinaingizwa kwenye mpango na kaya zisizo na sifa kuondolewa kwenye mpango.
Awali mpango wa kunusu kaya masikini awamu ya kwanza, uliozinduliwa mwaka 2012, umewezesha kuondoa umaskini kwa asilimia 10 mpaka 12 kwa kaya, huku tathmini ya jumla ikionesha mpango umefanikiwa kufikia adhma ya Serikali ya kuondoa umaskini uliokithiri kwa zaidi ya asilimia 82.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.