Uchimbaji wa visima viwili vya maji unaendelea kwa kasi katika shamba la mbegu Ilkiushini kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji unaotekelezwa na shirika la WaterAid jambo linaloashiri upatikani wa maji kwa wakazi wapatoa 50,000.
Mradi huo wa maji unatekelezwa kwenye vijiji vya Olkokola na Lengijave na vitongoji vya Olmotonyi, Ekenywa na Seuri vya Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5 kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza kupitia Idara ya Maendeleo ya Kimataifa 'DFID'.
Wakati huo huo serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeongeza kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kuongeza nguvu ya ujenzi wa mradi huo ili kWakatiuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwezesha kutumia chanzo cha maji cha Emutoto kilichopo kwenye msitu ndani ya hifadhi ya mlima Meru licha ya mradi huo kutumia vyanzo hivyo viwili vya kuchimbwa.
Mradi huo unategemea kukamilika mwishoni mwa mwaka huu 2018 na kuhudumia takribani wakazi 50,000 ambao watapata maji ndani ya mita 400 na kutekeleza mpango wa serikali ya awamu ya tano wa kuhakikisha asilimia 90% ya wakazi wa vijiji kupata maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.
Hata hivyo mradi huo utaambatana na teknolojia mpya ya kuchangia gharama za maji kwa kutumia mfumo wa kulipa kabla ya kutumia, mfumo unaojulikana kama eWaterpay utakaowekwa na shirika la eWater - Tanzania.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.