Vijana wa shule ya sekondari Musa, halmashauri ya Arusha, wameweka wazi kuwa, uelewa mdogo wa jamii hasa wazazi, juu ya afya ya uzazi, imekuwa ni chanzo cha ndoa na mimba nyingi za utotoni.
Wakizungumza wakati wa mdahalo wa Afya ya uzazi kwa vijana, uliofanyika shule ya sekondari Musa, mdahalo uliohusisha wanafunzi wote wa shule hiyo, wamesema kuwa, licha ya changamoto nyingi zinazowakabili vijana, bado uelewa mdogo wa vijana juu ya afya ya uzazi, umesababisha ndoa za utotoni na vijana kujikuta kwenye changamoto nyingi za kimaisha.
Wamefafanua kuwa, mara nyingi vijana hushauriana wao kwa wao, juu ya mabadiliko yao ya kimwili yanayoambatana na kuanza mahusiano ya kimapenzi, kwa kupeana taarifa zisizo sahihi, jambo ambalo husababisha mimba zisizotarajiwa pamoja na ndoa za utotoni.
Wameongeza kuwa, kutokana na mila na desturi za jamii zao, inaonesha wazi kuwa, hata wazazi hawana uelewa wa kutosha juu ya afya ya uzazi kwa vijana pamoja na mabadiliko ya kimwili kwa vijana jambo ambalo linasababisha vijana kubaki njia panda na pengine kushindwa kufikia malengo yao kwa kukatiza ndoto zao.
Wanafunzi hao wakwenda mbali zaidi na kusema kuwa, endapo wazazi wangekuwa na uelewa sahihi, juu ya afya ya uzazi kwa vijana, wasingewalazimisha wasicha kuolewa wakiwa na umri mdogo kwa kuhofia wasichana hao kupata mimba kabla ya ndoa.
Kadhalika katika mdahalo huo, vijana walipata fursa ya kujadili kwa kina juu ya afya ya uzazi na changamoto za mabadiliko ya kimwili zinazosababisha mihemko na namna ta kukabiliana na hisia.
Hata hivyo, halmashauri ya Arusha kupitia mradi wa TCI - TUPANGE PAMOJA , unaotekelezwa na shirika la JHPIEGO - Tanzania, wameanzisha huduma Rafiki kwa Vijana, huduma zinazotolewa bure kwenye zahanati na vituo vya afya na kuwataka vijana kwenda kwenye zahanati kupata elimu zaidi juu ya afya ya uzazi kwa vijana.
Afisa Afya Shuleni, halmashauri ya Arusha, Niya Mtaki akiongoza mdahalo juu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Musa
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Musa wakifuatilia mijadala kwenye mdahalo wa afya ya uzazi kwa vijana uliofanyika shuleni hapo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Musa wakijifunza kwa picha namna ndoto zao zinavyokatizwa wakati wa mdahalo wa afya ya uzazi kwa vijana uliofanyika shuleni hapo.
Mratibu mradi wa afya ya uzazi na Uzazi wa Mpango shirika la JHPIEGO, Waziri Njau, akitoa mada juu ya Uzazi wa Mpango na dini za kikristo na kiislam, wakati wa mdahalo wa afya ya uzazi kwa vijana, shule ya sekondari Musa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.