Mkurugenzi wa Halmashauri yaWilaya ya Arusha, bwana Suleiman H. Msumi ( wa pili kutoka kushoto aliyevaa Kaundasuti) akiwa na Mratibu wa Miradi toka Shirika la Habitat for humanity Tanzania bi.Enoti Lekaaya( wa pili kutoka kulia) pamoja na timu ya waratibu wa mradi wa ujenzi wa vyoo vya kisasa unaotekelezwa kwenye masoko ya olmotonyi na Oltrumet.
Mradi huo wa vyoo vya kisasa unatekelezwa na shirika la WaterAid chini ya ufadhili wa Shirika la Habitat for Humanity Tanzania ukiwa na lengo la kuboresha vyoo kwenye masoko ili kuisaidia jamii inayotumia masoko kujipatika kipato kuwa salama hususan Wanawake ambao ndiyo walengwa wakuu wa mradi huo.
Shirika la Habitat for Humanity limeridhishwa na maendeleo ya mradi pamoja na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha,bwana Suleiman H. Msumi kwa ushirikiano anautoa katika kutekeleza mradi huo ndani ya Halmashauri yake.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.