Ujenzi na Upanuzi wa miundo mbinu ya Kituo cha Afya Nduruma unaendelea vizuri miezi miwili baada ya halmashauri kupokea fedha kiasi cha Shilingi milioni 500 kutoka Serikali kuu.
Fedha hizo zimetolewa na Serikali kwa lengo la kuhakikisha kituo hicho kinakuwa na hadhi ya Nyota tano na kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha Afya chenye hadhi hiyo.
Kiasi hicho cha fedha kinatumika kujenga jengo la Maabara kwa ajili ya vipimo, jengo la Mama na Mtoto 'Maternity Ward', jengo la kuhifadhia Maiti 'Mortuary', jengo la kuchomea taka 'Incinerator', nyumba ya Mganga pamoja na umaliziaji wa jengo la upasuaji 'Operation Theater'.
Hata hivyo ili kuhakikisha fedha hizo zinakamilisha ujenzi huo kwa wakati na gharama nafuu, Halmashauri ya Arusha imelazimika kutumia Mafundi wa kawaida na sio Mkandarasi njia inayojulikana kama 'Forced Account' kulingana na kanuni za manunuzi.
Kituo hicho cha Afya kinategemea kuhudumia wananchi wa kata ya Nduruma na kata za jirani za Bwawani, Mlangarini na baadhi ya maeneo ya Jiji la Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.