• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Ujenzi wa Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule waanza Arusha DC

Posted on: July 3rd, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Moja ya mikakati ya Serikali ya awamu ya tano, ni kuweka mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia pamoja na usimamizi imara wa kuthibiti ubora wa shule, lengo likiwa ni kupandisha kiwango cha taaluma kwa shule, kwa kuweka mazingira rafiki kwa walimu, wanafunzi na wasimamizi wa elimu.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi, Ufundi na Teknolojia, inaendelea kutetekeleza mikakati hiyo, kupitia miradi ya Lipa Kutokana na Matokeo (Education Payment for Result' ‘EP4R’), kwa kuanza kutekeleza miradi ya ujenzi wa Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule kwenye Halmashauri zake.

Halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa Halmashauri 100 Tanzania, zilizopata fedha kiasi cha shilingi milioni 152,  fedha za Serikali kupitia miradi yake ya  ‘EP4R’, ujenzi utakaogharimu kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule, Ofisi ambayo kwa kiasi kikubwa, itatatua changamoto ya msongamano wa wafanyakazi wa wa kitengoe hicho.

Mhandisi wa Ujenzi Halmashauri ya Arusha, Mhandisi Bibie Manzi, amesema kuwa, mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya Ofisi hiyo ya kisasa, uliozingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu, upo katika hatua za awali, mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 152, na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Augusti 2019, ukiwa umejumuisha vyumba vinne vya ofisi, ukumbi mdogo wa mikutano, jiko, vyoo pamoja na vyoo maalum kwa ajili ya watu wenye walemavu.

Akizungumza na mwandishi wetu, Mdhibiti Mkuu Ubora wa Shule, Halmashauri ya Arusha, Mwalimu Fatuma Lema, amesema kuwa, mradi huo wa ujenzi wa Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule, katika halmashauri hiyo, umekuja wakati muafaka, kutokana na ufinyu wa ofisi iliyokuwa ikitumiwa na kitengo hicho kwa muda mrefu sasa, jambo ambalo lilisababisha kukwamisha ufanisi wa kazi.

“Kukamilika kwa mradi huo, kutaondoa changamoto nyingi zilizokuwa zinatokana na ufinyu wa ofisi tuliyokuwa inatumika, na zaidi kutaongeza ufanisi katika kazi za usimamizi wa utoaji elimu na kuthibiti ubora wa shuleni, pamoja na kuongeza ushirikiano baina ya wafanyakazi kwa kukaa kwa pamoja’amesema mwalimu Lema.

Akieleza shughuli zinazofanywa na kitengo cha Uthibiti Ubora ngazi ya halmashauri, mwalimu Lema, amefafanua kuwa, Kitengo cha Uthibiti Ubira wa Shule, ni dira ya elimu katika shule, kinachojishughulisha na  kusimamia Sera ya Uthibiti Ubora wa Shule,  kwa kusimamia ubora wa shughuli zote zinazofanywa shuleni, ikiwemo njia na mbinu sahihi za kufundishia, kufundisha kwa kufuata mitaala ya elimu, kuandaa masomo na nukuu za somo, pamoja na mazingira yote ya kujifunzia na kufanya tathmini ya ubora wa taaluma inayotolewa shuleni na kufanya tathmini ya kiwango na ubora wa elimu.

"Kitengo cha Uthibiti Ubora ni kitengo nyeti, kwani ndio Dira ya ubora wa shule, chenye jukumu la kusimamia utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi, matumizi ya mbinu sahihi za kufundisha na kujifunzia pamoja na kufanya tathmini ya ubora wa taaluma inayotolewa shuleni" amefafanua mama Lema.

Aidha mwalimu Lema, ameipongeza Serikali ya awamu ya tano, kwa kuona umuhimu wa kitengo cha Uthibiti Ubora wa Elimu, kwa kujenga ofisi, jambo ambalo halikuwahi kufanyika hapo awali, na kusababisha watumishi wa kitengo hicho, kujibanza kwenye ofisi za elimu.

Mwalimu Lema hakusita kumshukuru Murugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera pamoja na ofisi ya Mkuu wilaya ya Aumeru kwa kukubali kutoa eneo la kujenga Ofisi hiyo, sharti ambalo lilitolewa na Serikali, pamoja na ushirikiano wa hali ya juu wakati wote wa mchakato wa utekelezaji wa mradi huo.

Serikali kupitia miradi ya EP4R inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia, imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.5, kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule, kwenye Halmashauri 100 za Tanzania.

Ujenzi wa Ofisi hizo ni utekelezaji wa Sera ya Elimu bila Malipo, inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano, kwa kuboresha miundombinu ya elimu nchini, kwa lengo la kupandisha kiwango cha taaluma, na kurejesha hadhi ya shule za Serikali, iliyokuwa ikiendelea kupotea, kwa kuwezesha mazingira bora ya kujifunza na kufundishia na utoaji wa huduma ya elimu bora, mkakati ambao umeanza kuleta mafanikio chanya katika sekta ya elimu hususani uboreshaji wa miundombinu nchini.
















Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.